Wazee Vipi Hii:- Eti Sikinde Imekufa Au?

Wazee Vipi Hii:- Eti Sikinde Imekufa Au?

Joined
Apr 27, 2006
Posts
26,584
Reaction score
10,400
Buriani sikinde ngoma ya ukae

- mwanzo ilikuwa kama utani pale redio mbao zilipoanza kutangaza kwamba wamiliki wa bendi ya mlimani park orchestra wana sikinde ngoma ya ukae, shirika la mandeleo mkoa wa dar (DDC) wako njia moja kuivunja bendi hiyo kwa kile kilichosemekana kwamba ni mzigo kwa shirika hilo.

- wiki hii imethibitika kwamba habari hizo za kutia uchungu ni za kweli.
hivi tunavyoongea wanamuziki wa sikinde ama nginde nginde hawana ajira, ila inasemekana mwajiri wao amewapa mkono wa dhahabu kwa kuwakabidhi vyombo vya muziki wakajiajiri wenyewe, kama ilivyo msondo ngoma band ambao walijikuta katika jahazi kama hilo baada ya mwajiri wao, jumuiya ya wafanyakazi, kuitema.

- Macho na masikio ya wapenzi wa muziki yanangoja nini kitachofuata, japo wengi wana imani kwamba sikinde haitokufa kutokana na kusheheni nyota wa muziki kama vile hassan rehani bitchuka 'super stereo, na mkongwe shaaban dede.
 
Mkuu, kama wameachiwa vyombo basi naamini hawatakuwa tayari kuiua 'nginde ngoma ya ukae' ni moja ya bendi ambazo muziki wake ulikuwa na bado unavutia sana na nyingi ya nyimbo zao kama unaisikia redioni na ulikuwa unataka kutoka basi huweza kuvunja safari yako ili kuusikiliza wimbo huo mpka uishe.

Nimecheza sana nginde katika mikoa mbali mbali ya Tanzania na sitafurahia kabisa kusikia haipo tena katika Ulimwengu wa muziki.
 
Yaani wakati huu ambao tunajitahidi kupigia debe muziki wetu wa "Kitanzania", hilo shirika la "DDC" limeamua "SUPU KUITIA NAZI.....!?"
Kwa kweli mimi ni mmoja wa mashabiki wakubwa wa SIKINDE NGOMA ya ukae ambao nimeshtushwa sana na uamuzi huu!
Ninaamini watatokea wadau wa muziki ambao hawatakubali kuona wanamuziki wetu mahiri, Bitchuka, Dede, Ngosha, Mapesa, Milambo na wengine wengi wanatoweka katika ulimwengu huu wa muziki!!!
 
Nafikiri Sikinde ni wakati muafaka wa kujifunza jinsi gani ya kujitegemea; huwezi kujua.... labda huu ndio wakati muafaka wa maisha ya wanamuziki wa Sikinde kubororeka; kwani najua kuna watu/taasisi mbali mbali ambazo walikuwa wanataka kuingia mktaba na Sikinde lakini ilikuwa vigumu sababu ilikuwa inamilikiwa na DDC; so kinachotakiwa ni wanamuziki kuwa serious into business; wasiwe na tamaa ya pesa; of course mwanzoni watapigika kidogo lakini wakitulia na upngozi mzuri wakatafuta wadhamini nafikiri Sikinde watafika mbali otherwise SIFAGILLII KABISA SIKINDE KUFA, kwani sasa ni bendi mbili tu ambazo zinabeba litma ya Kitanzania MSONDO na SIKINDE; kwani bendi nyingi aidha zimekufa au zimemezwa na litama ta kizaire
 
duniani kuna mambo,wanapokuona umkimya,watakufuatafuata na maneno ila wakupe sifa mbaya,hata ukifanya jambo zuri,wao watakukashifu,kwa vile wameshazoea kusema,eheh waseme mwisho watachoka,waache waseme mwisho watachoka,ngoma ya sikinde tutaiendeleza,walimwengu tuacheni manenomaneno,tutazama dunia hii inapokwenda mbele,kusemanasemana hakuna maana yoyote nawaombeni walimwengu tushirikiane jamani hiii! jamani nimeikumbuka sana hii nyimbo mwenzenu
 
Hizi habari ni nzito kuzisikia kwa mtu anaependa kuonekana pale old Trafold kila J2 mana ndio palikuwa pakumalizia weekend kwa kupata vibao vya wananginde..Binafsi ni mpenzi mkubwa wa sikinde..sintosahau miaka 21 ya sikinde 1999 pale DDC -KARIAKOO kwa udhamini wa bia ya KIBO GOLD ilikuwa show moja baaakubwa ila kumbukumbu haswa ambayo iliniwekea historia ni baadaya ya show kwisha..sikumbuki T shirt waliyotoa na cassette vilipotelea wapi!!...Ila umefika wakati sasa bendi kujiendesha kibiashara ingawa ni ngumu sana kwa mziki wa Bongo...Wakajipange nao watoke kama Wanamsondo ngoma
 
Ni sawa na kumuua Nyoka halafu usimkate ndosi.
Nginde litaendelea kusimama kama liliposimama mwaka ule baada ya MV Mapenzi kupigwa na Dhoruba na hatimae nahodha akajitosa Baharini.

Nani anaweza kumtaja huyo NAHODHA aliyejitosa?
 
Back
Top Bottom