Mkuu, Kutokana na nukuu hiyo ni kuwa self defense inaweza kuwa perfect au sio perfect. Ni sawa kabisa. Kwa maneno mengine, au kwa tafsiri, nukuu hii inajikita katika dhana inayobeba neno
self defence katika maana yake halisi kama utetesi mahakamani. Ili self defense ikubalike katika mahakama kuwa genuine na ilikuwa na ulazima kutakana na mazingira ya tukio, ni lazima ikidhi vigezo vifuatavyo kwa uchache:
- Isitokane na gubu la ugonvi au chuki lililokuwepo awali kati ya mtuhumiwa na marehemu. Hapa ina maana kwamba self defense inatakiwa iwe mpya, au tukio la dharula kwa maana nyingine. Hakuna self defense itakubalika kama wahusika walishawaki kuwa na migongano au ugonvi unaofanana na tukio la mwisho lililopelekea kifo.
- Isifanyike katika mazingira ya ugonvi wa moja kwa moja. Mfani ni kama wawili wanapigana, mmoja akaamua kutumia nguvu ya ziada kummaliza mpinzani wake.
- Nguvu ya kupindukia haitakiwi. Nguvu hii ikitumika katika self defense inaua kabisa dhamira ya self defense.
- Self defense inatokea pale tu mtu anapotetea uhai wake, sio mali au uhai wa mwingine.
Kuhusu suala la binti huyu, ushahidi wa moja kwa moja katika mazingira ya tukio unakosekana sababu tukio lilitokea wakiwa wawili. Uzuri mwingine hakuna ushadi kuwa mtuhumiwa alimshambulia marehemu au alitumia nguvu iliyopindukia katika kujitetea. Kwa maana hiyo mtuhumiwa anao utetezi perfect self defense (au alikuwa na wasaa wa kuipa mahakama utetezi huo).
Self defense ikitetewa vyema inaweza kufanya mahakama imuachie huru muuaji! Hata hivyo inahitaji wakili mzuri katika utetezi tokea hatua za awali za kesi/mashtaka. Wengi wanakosea kuweka utetezi huu mbele ya mahakama na mwisho unaishia kusaidia kubadiri kosa na kupunguza adhabu tu.