Wazee wa fix ni noma

Fix fix ni muhimu joo...... tueleze basi kwanza wewe ulipigwa wapi fix
Na kweli ww kwa fix ni hatari!

Wakija watie fix hadi walainike[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Bila fix haupatii vizuri""mimi nakumbuka nlimpiga fix mtto wa college kuwa ni Dakitare kumbe ni Butcherman akaingia king nikamgege..[emoji23][emoji23]
 
Kipindi hiki ajira ngumu akatokea jamaa tulisoma naye O level akasema mjomba ake ana ishu ya kutulink na Tanesco elimu inayohitajika ni form four tu.

Ila inahitajika tumpe 73k na watu wanahitajika haraka mno ndani ya wiki 2 nafasi ziwe zimejazwa, kuanzia hiyo siku tuliyopata mchongo, mshahara 600k.
Mi hua fasta sana kudetect scam na scammer. Sheria kuu ni hii "Ukiona mchongo ni mtamu kuliko utamu wenyewe achana nao" sasa 73k kwa 600k ni mchongo mtam mno, kufikia hapo nikadetect hii ni scam.

Wadau tukaomba kuonana na jamaa, akaja. Nikaangalia mavazi, namna anavyoongea na ndevu zake alivyoamua kuzitunza na jinsi anavyojibu maswali (alikua anakazana sana na neno "Niaminini mimi" "Mnaweza kuja hata ofisini", tukaachana naye. Tukabaki wadau sita tunaotaka hizo nafasi tukaanza kujadiliana.

Tukamuuliza yule rafiki yetu mjomba wako una uhakika anafanya kazi Tanesco? Akajibu hua anaonana naye kwa babu tu hua hana stori naye na alicheki na shangazi yao akasema anavyojua jamaa anafanya kazi Coca. Lakini pia jamaa anaishi kwa kujitenga mno.

Tukamwambia mpange jamaa kua hii 73k siyo kubwa sisi tunataka tumpe shukrani kubwa, atuache tuingie kazini tutagawana naye mshahara. Jamaa akagoma.
Tukasema basi tukupe hiyo 73k tukiingia ofisini akagoma pia kwa madai mkono mtupu haulambwi.
Kufikia hapa nikakamilisha kua huyu ni scammer, unakataaje 1.8m over 438k? Nikawaambia wadau huyu mwana hafai.

Wakajibu ila 73k ni ndogo, nikasema zikishakua nyingi hazitakua 73k, mmoja akajibu jiangalie wewe ulichotoa siyo na cha wenzako. Nikamuuliza akienda dukani akiambiwa hii feni ni 80k atasema hawezi kununua kwakua ana 73k ya Castr na hawezi ichanganya na yako?

Mi nikasema hii deal mi najivua. Wana wakasema we are giving it a try nikawajibu poa.

Kesho yake wakampelekea jamaa pesa na cv zao, hiyo ilikua mwezi wa 3 mpaka leo wanazungushana na yule bwana.

NB. Kama tulikua wote pale kikaoni siku ile tafadhali usitaje jina langu hapa, wala usije pm.
 
Kuna mzee mmoja nuksi sana lakini akiongea ni kama malaika anavyofix vitu unaeza ukaamini nuksi zote zinaisha kumbe ameshamwaga nuksi tupu, fix zingine bhana huchomoki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaa hapo mwisho umemalizia fresh sana

Sasa hiyo 73k ndo nini mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasiasa ndio wanaongoza kwa fix...

Wakati wa kuomba kura aisee unaweza ukadhani jamaa akichaguliwa raia tutakuwa tunakinga maziwa bombani...

Shubaaaamit ngoja awe kiongozi sasa, kupata maji hadi mvua inyeshe...
 
Wanasiasa ndio wanaongoza kwa fix...

Wakati wa kuomba kura aisee unaweza ukadhani jamaa akichaguliwa raia tutakuwa tunakinga maziwa bombani...

Shubaaaamit ngoja awe kiongozi sasa, kupata maji hadi mvua inyeshe...
Taja japo mwanasiasa mmoja ambaye ni mzee wa fix

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…