Wazee wa kazi kuelekea katikati ya jiji, kulikoni?

sawabho

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Posts
5,286
Reaction score
3,111
Kwa wana JF mliokatikati ya Jiji la Dar es salaam tujuze, nimekutana hapa TAZARA na magari manne ya wazee wa kazi yaani Field Force Unit a.k.a Fanya Fujo Uone (FFU) na Washa washa moja yakielekea kati kwa speed kali, kulikoni huko?
 
Nadhani watakuwa wanawafuatilia wazee wa afrika mashariki kazi ipo kweli wajukuu wanawafanyizia mababu na mabibi.
 
Jk nae si awalipe tu yaishe jamani aah tumechoka banaa
 
Kuwaita wazee wa kazi ni kuwapa sifa wasiyostahili hawa vichwamaji.

Wakati mwingine wanafanya kazi nzuri, pale wanapofanya kazi nzuri tuwape sifa na pale wanapofanya vibaya tuwalaani. Angalia hali ya ujambazi imetulia kidogo.
 
Nadhani watakuwa wanawafuatilia wazee wa afrika mashariki kazi ipo kweli wajukuu wanawafanyizia mababu na mabibi.

Hawa wazee walishabugi ma step, walitakiwa kusimamia haki zao wiki mbili kabla ya uchaguzi mkuu - wangeshalipwa pesa zao, ila kwa sasa kulipwa ni ndoto, watapigwa washawasha mpaka wakumbuke ahadi za mwana TANU.
 
Kuwaita wazee wa kazi ni kuwapa sifa wasiyostahili hawa vichwamaji.

hawa naona hawana makali ya maisha nini? maana wanapiga kazi kwa moyo - inaonekana salary scales zao ni tofauti na hizi za kwetu.
 
Wakati mwingine wanafanya kazi nzuri, pale wanapofanya kazi nzuri tuwape sifa na pale wanapofanya vibaya tuwalaani. Angalia hali ya ujambazi imetulia kidogo.

taja mojawapo ya kazi nzuri waliyowahi kufanya in the last two years! usitaje kuhusu kulinda mabenki maana hiyo jeshi linalipwa na mabaenki!
 
hawa wazee si ndo wale walokuwa wanasikiliza speech ya mbayuwayu na kupiga makofi watoto wao wanaofanya kazi serikalini wasiongezewe mishahara? hawajui timing hawa
 
hii nchi sasa!kila mahali grievances!kuna anayetamani kuzika mumewe kwa amani,kuna anayetaka kapensheni kake.mie macho yamenitoka kwa kiu ya nyongeza ya mshahara!aaah,ngoja tuone!
 
Wamepata uhamisho, wanaenda mkoa wa kipolisi wa Tarime. Ni dharura, so mizigo na familia zao vitafuata huko huko baadaye!
 
Wakati mwingine wanafanya kazi nzuri, pale wanapofanya kazi nzuri tuwape sifa na pale wanapofanya vibaya tuwalaani. Angalia hali ya ujambazi imetulia kidogo.

Sio wao ndio wameacha/wametulia kwanza! kwani unafikri hizo ak 47 majambazi wanapata wapi?
 
Jk nae si awalipe tu yaishe jamani aah tumechoka banaa

siyo kwamba hataki kuwalipa, wewe hujui hazina imebaki while denti?

tusimlaumu sana ni mfumo umezeeka na umeshindwa kufanya kazi, yaani kila sekta ni madudu tu.
 
Jibu sahihi la muuliza swali bado kujibiwa anapenda kujua ffu wanenda wapi na kufanya nini naona wengi wanakisia badala ya kujibu swali.
 
taja mojawapo ya kazi nzuri waliyowahi kufanya in the last two years! usitaje kuhusu kulinda mabenki maana hiyo jeshi linalipwa na mabaenki!

Kuwadhibiti wafanya fujo Arusha.
 
Wamepata uhamisho, wanaenda mkoa wa kipolisi wa Tarime. Ni dharura, so mizigo na familia zao vitafuata huko huko baadaye!

nilikua mgumu kucheka tangu juzi, Thank u great thinker.
 
JK hana pesa za kuwalipa wazee serikali imefirisika mfano Wanajeshi hapa Arusha hawaendi kazi kwa sababu ya ukata, wanaonda niwale wanao bahatika kudandia mabasi ya Mtei lakini malori yao yamepark hayana mafuta itakuwa za kuwalipa wazee.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…