LGE2024 Wazee Wa Kigoma Wafanya DUA Maalumu Uchaguzi Serikali Za Mitaa kwa kuchinja ngamia

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
29,909
Reaction score
32,414
Wazee wa ACT Wazalendo Kigoma Waufuatilia Uchaguzi Kwa Namna Yao, ‘Dua’.

Ikiwa zimebaki siku nane kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mnamo Novemba 27,2024, wazee wa ACT Wazalendo mkoani Kigoma wamefanya 'dua maalum' kwa ajili ya yeyote atakayehusika na kujaribu kuharibu uchaguzi huo.

Dua hiyo iliyoanza asubuhi ya leo Novemba 19, 2024, na kumalizika mchana kwa kuchinja ngamia inaelezwa kuwagusa moja kwa moja wadau mbalimbali watakaoshiriki katika uchaguzi huu ambao wazee hao wanaona ni muhimu sana kwao.

Akiongelea juu dua hiyo Msemaji wa ACT Wazalendo Masuala ya Uchaguzi Serikali za Mitaa, Rahma Mwita amesema wanachama hao wameamua kufanya kile wanachoona kinaweza kulinda haki zao.

"Chama ni cha wanachama, baada ya wao kuona kuna mambo yasiyofaa kwenye uchaguzi wameona watumie njia hiyo," Rahma aliambia The The Chanzo katika mahojiano.

Soma Pia:
Kwa mujibu wa wazee hao, hii si mara ya kwanza wao kuufuatilia uchaguzi kwa kutumia 'dua' na wamekua wakiona matokeo stahiki.

Snapinsta.app_467530285_853978633481825_442668657112557322_n_1080.jpg
 
KIFUA KIPANA ajiandae.
Nimefurahi sana kwa wazee hao kuombea nchi yetu amani na upendo katika uchaguzi.

Huo ndio uzalendo wa kweli sasa.

Dua ndiyo dawa ya chuki binafsi, gubu, mihemko na makasiriko ya wanaopenda mbeleko 🐒
 
Huo ndio uzalendo kazi ya hiyo dua kila ataweka kura zaidi ya moja na yeyote atakae subutu kumtangaza ambaye sio mshindi basi amekwenda na maji
 
Nimefurahi sana kwa wazee hao kuombea nchi yetu amani na upendo katika uchaguzi.

Huo ndio uzalendo wa kweli sasa.

Dua ndiyo dawa ya chuki binafsi, gubu, mihemko na makasiriko ya wanaopenda mbeleko 🐒
Subiri matokeo
 
Wazee wa ACT Wazalendo Kigoma Waufuatilia Uchaguzi Kwa Namna Yao, ‘Dua’.

Ikiwa zimebaki siku nane kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mnamo Novemba 27,2024, wazee wa ACT Wazalendo mkoani Kigoma wamefanya 'dua maalum' kwa ajili ya yeyote atakayehusika na kujaribu kuharibu uchaguzi huo.

Dua hiyo iliyoanza asubuhi ya leo Novemba 19, 2024, na kumalizika mchana kwa kuchinja ngamia inaelezwa kuwagusa moja kwa moja wadau mbalimbali watakaoshiriki katika uchaguzi huu ambao wazee hao wanaona ni muhimu sana kwao.

Akiongelea juu dua hiyo Msemaji wa ACT Wazalendo Masuala ya Uchaguzi Serikali za Mitaa, Rahma Mwita amesema wanachama hao wameamua kufanya kile wanachoona kinaweza kulinda haki zao.

"Chama ni cha wanachama, baada ya wao kuona kuna mambo yasiyofaa kwenye uchaguzi wameona watumie njia hiyo," Rahma aliambia The The Chanzo katika mahojiano.

Soma Pia:
Kwa mujibu wa wazee hao, hii si mara ya kwanza wao kuufuatilia uchaguzi kwa kutumia 'dua' na wamekua wakiona matokeo stahiki.

View attachment 3156313
Pamoja na yote hebu turudi pale Rau madukani😂

Wale watekaji walioonekana kwenye ile clipp wameshakamatwa? Au ndo tunasahaulishwa hivyo?
 
Asubuhi tutaona nazi zimevunjwa kwa mamia njia panda zote za Kigoma
 
Nimefurahi sana kwa wazee hao kuombea nchi yetu amani na upendo katika uchaguzi.

Huo ndio uzalendo wa kweli sasa.

Dua ndiyo dawa ya chuki binafsi, gubu, mihemko na makasiriko ya wanaopenda mbeleko 🐒
Gentleman, kwenye uchaguzi huu mimi na wewe tutachuana vilivyo.

Nimezindikwa kweli kweli mpaka kwenye visigino.

Jiandae kulamba mchanga Gentleman.
 
Pamoja na yote hebu turudi pale Rau madukani😂

Wale watekaji walioonekana kwenye ile clipp wameshakamatwa? Au ndo tunasahaulishwa hivyo?
Umeongea jambo jubwa sana..
Hata sativa aliwataja waliomteka
Bobge alietaka kutekwa juzi watekaji cctv camera ziliwanasa.
Kakini kama taifa tuna ombwe ktk kufikiri..
Na pia tu ashida ya usahulifu
 
Gentleman, kwenye uchaguzi huu mimi na wewe tutachuana vilivyo.

Nimezindikwa kweli kweli mpaka kwenye visigino.

Jiandae kulamba mchanga Gentleman.
hujajiandikisha lakini unajipiga kufua hivyo gentleman?

ushirikina kitu mbaya sana aisee,
dah! nimeshangaa kijana mtanashati kabisa lakini kabeba hirizi kiunoni ?🤣
 
Wanachama wa ACT WAZALENDO wamefanya dua ya kuchinja ngamia kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mambo makubwa waliyosema ni kwamba kumekuwa na tabia ya kukata majina ya wagombea na kutangaza mtu ambaye hajashinda safari hii Kila kitu wamemwachia Mungu ndiye ataamua ugomvi.

Back
Top Bottom