Siku moja nilikua Nyegezi Mwanza kuna bar jirani na nilipokuwa naishi. Kuna mhudumu nilimkuta analia....mtoto mzuri wa Kimbulu na lafudhi yake ya kwao. Analia na kulalamika kwa jamaa mwenye tabia ya kugomea kulipa bill zake...anaweza kunywa 5 akadai amepiga 2 tu na anagoma kweli na halipi. Yule mhudumu akawa analia siku hiyo tena akakatwe mshahara....anasema "unadhani mi nimetoka Karatu kuja kujiuza hapa, nitaishije mie...kila siku mshahara unakatwa...mwisho wa mwezi sina kitu. Nijiuze ndio niishi...maisha haya mpaka lini? Siwezi kwa kweli leo utalipa...hapana sijaja hapa kujiuza."
Huruma ikanijia...nilikua na wahuni wangu tulimkwida jamaa akalipa.
Kadem ni kazuri balaa.