Wazee wa mila waamua kuisimamisha mvua mkoani Ruvuma hadi siku ya mazishi ya Jenista Mhagama

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Baraza la Wazee wa Mila na Desturi mkoani Ruvuma limetangaza uamuzi wa kuisimamisha mvua isinyeshe kuanzia leo Desemba 13, 2025 hadi Desemba 16, 2025, siku ambayo aliyekuwa Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, atazikwa.

Uamuzi huo umefikiwa kufuatia mvua iliyonyesha asubuhi ya leo, Desemba 13, 2025, katika makazi ya marehemu Jenista Mhagama yaliyopo eneo la Makambi, Manispaa ya Songea.

Baraza hilo limesema hatua hiyo imelenga kutoa heshima ya mwisho kwa marehemu na kuhakikisha shughuli za msiba na mazishi zinafanyika bila usumbufu wa hali ya hewa.

Upuuzi mtupu, ule ule wa Majimaji na risasi zitayeyuka, wakapukutika. Isiponyesha ni coincidence na si vinginevyo
 
Wakazi wa Ubungo watalia sana wakisoma hii habari.
 
wao wazee wa mira wajajua aliyemuua mtu wao
 
Wapeleke mwanza na dar maana wamedai maji yameadimika kutokana na mvua kutokuwepo
 
Mara paaapu! Wapo katikati ya maombi mvua hiyo inashuka na kulowanisha ndevu zao.
 
Back
Top Bottom