Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

mkuu mbona unaua ndoto Makati umri bado unasoma?
Siyo kuuwa ndoto naangalia income yangu kwa mwaka na bei ya RR mpya na ushuru wake plus maintenance costs.Hata kama ntalimiliki on finance kwa maana mikakati mingine isifanyike mshahara wote ukija 95% unaenda kwenye makato ya gari,nina rafiki mmoja anayejiweza analo moja on finance alinishauri kama kipato chako ni cha mtu wa kawaida nisijiroge kuchukua on finance na ndipo ndoto zikafa.Mpaka kibubu kiwe full kulinunua cash uzeeni haina maana.
 
Ivi hii chuma na ile ya mtoto wa Tandale ( cadillac escalade black edition ) ipi moto 🙂🙂🙂
Extrovert
Escalade yenye V8 6.2L ni yamoto kuliko hii Land Cruiser japo wamepishana horsepower kidogo sana! Escalade inamwaga 420HP wakati huu umeme wa Mjapani unamwaga 410HP so difference haitakuwa kubwa sana isipokuwa tu kwenye speed escalade ana 280 kwenye kisosi!😅😅😅 huku LandCruiser ana 260!

Ila Escalade ya V6 3.0L ni ya kitoto sana ina 277HP wakat landcruiser ya v6 3.0L inamwaga moto wa 310HP so Land cruiser ataiburuza escalade ya 3.0L
 
Ila Escalade imekaa kitemi mno kuliko Cruiser
 
Ivi hii chuma na ile ya mtoto wa Tandale ( cadillac escalade black edition ) ipi moto [emoji846][emoji846][emoji846]
Extrovert
I think cadillac is a more of a status car, more luxury. LC ni luxury na wakati huohuo ni kazi kazi yani popote inaenda na kukurudisha. Nguvu almost the same. Ila cadillac ni gas guzzler.
 
Ubaya wa gari za marekani.

Engine kubwa, output ndogo.

Yani 6.2l v8 inakupa 420 hp wakati Merc Benz A 45s AMG ana 2l inatoa 421 hp.

Wamarekani wanawezana wenyewe.
 
Ubaya wa gari za marekani.

Engine kubwa, output ndogo.

Yani 6.2l v8 inakupa 420 hp wakati Merc Benz A 45s AMG ana 2l inatoa 421 hp.

Wamarekani wanawezana wenyewe.
Hahahah mjeruman ataki tabu yeye ni kufunga ma turbochargers tu😅😅😅!!! Hilo li engine la 6.2L unakuta lenyewe ni naturally aspirated.

Toyota nae ameamua kuwa nzi mwenye akili kama nyuki anafyatua zenye turbo tu sahizi ameacha uoga!
 
Wamarekani wanakwambia only milk comes with 2L.

Mafuta cheap sana kwao kulinganisha na Europeans. Halafu wana hela.

Ndo maana kwao kukuta gari la 7.3L ni kitu cha kawaida sana.

Wana hiyo Ford Mustang shelby gt500 5.2l v8 supercharged inakupa 720hp. Gari ina sura ya kikatili sana.
 
Hahahahah kumbe ndio maana wanainjoy ma gas guzzlers
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…