Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Ila mnaosafiri usiku nawaelewa maanake foleni nimeanzia Ubena zomozi hadi Moro nyuma ya malori! Ukiovateki kijinga unakula cheti! Nimetumia masaa mawili Chalinze-Morogoro
Yani kuna sehemu unaona kabisa hapa naweza kupita, tena very safely, nikaendelea na safari. Ila ukiwaza itakucost shs ngapi unatulia kinyonge.

Unaweza kumlaani aliyechora mistari na kuweka vibao barabarani.
 
Mrejesho... wa gari lisiilo na speed o meter na halichanganyi mwendo haraka.
Nnilitoka dar saa 10:47 usiku- kupitia msoga nikafika moro saa 2:14. Nimeondoka moro saa 2: 55 baada ya kula vichwa vya kunipa company...nimefika dom saa 6:17 asubuhi. Top speed ilikua 110 ndo uwezo wa gari unapo ishia... Kwa kutumia app ya simu yenye speed o meter.
Kwa mtazamo wangu njia ya msoga ni ndefu kulinganisha na njia ya baobab kutokea mile 1. Yote kwa yote nimefika salama na mshukuru mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…