Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Sishangai Maana mtu kasajiiri 812 Leo na Mwisho Ni 999, Maaninah zinakimbia kama upepo

Sio Mbaya tunafungia Mwaka 2020 na DVE, sijua tutafungia 2021 na ipi ?View attachment 1663246
Kifuatacho soon tutaingia namba E....Basi hawa wa Namba E watakuwa wanaona Dunia nzima ni yao....utakutana na Porte namba E jamaa kavaa miwani nyeusi, kakata kishoka, ndevu kaziachia kama brush....yaani atatuona tuliobaki wote ni washamba tu..[emoji848][emoji848]...akisimamishwa na askari, ataongea kwa kiburi cha namba E, basi askari hapo anachora vyeti tu.

Hawa wenye D wataanza kujiona kama sisi wenye C tunavyojiona leo hii..

Wenye C tutajiona kama wanavyojiona wenye B leo hii..

Wenye B watajiona kama wanavyojiona wenye namba A leo hii...

Wenye namba A watajiona wamerudishwa enzi za namba TZ 009844[emoji21]

Wale ambao waliwahi kuwa na namba TZ.......watajihisi wanaishi on the other side of the hell....[emoji26][emoji26]

Ndiyo Tanzania hii imetawaliwa na Plate namba na Low mileage..
 
Dah we jamaa bhana Nimechemka duh
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Lakini Kuna vyuma namba A vinaita achaa ving'wasuuu, Cheki hio CRUISER hapo
 
Vinaita balaa...lajini usishngae mtu akatoa Passo yake bandarini ya pistoni tatu ikasajiliwa namba E....akaaza kuvimbishiana na Hiyo AAA hapo..[emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23]

Kuna verosa nineiona jana hapo Kibo ni IT kidogo nilie. Kwani huwa magari mabovu yanauzwagwa jaman? Au lilikaa juani sana hapo bandarini? Lkn pia hapana. Ilikua zaidi ya kupauka. Hapo mbele limeishaa[emoji119][emoji119] imagine ndo namba E
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Isijekuta limekaa sana bandarini akatokea mtu akajikomboa nalo..
 
Wengine hununua haya kwa bei nafuu hlf wanakuja kuyafanyia repair.
 
Mungu ni mwema nimevuka salama na hatimaye Kuuona mwaka 2021..

Ninaimani wazee wote wa road trip mmevuka salama..

Mungu awatangulie katika kutimiza malengo ambayo hayakutimia kwa mwaka uliopita wa 2020..

1.Wakuoa aoe.
2.wa kuolewa aolewe
3.Wakuachika asiachike tena
4.Wa kutafuta kazi/biashara/masomo afanikiwe
5.Ndoto ya Ujenzi/kiwanja/gari ikatimie.

Mapambano yanaendelea.
View attachment 1664315
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…