Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Huo mtaa upo wapi?

Inawezekana napita ila sipafahamu.
Ukiwa unatokea hii barabara inayotoka Dar express kushuka kama Idara ya maji, utafika junction ya pale Cafe laziz, iache endelea mbele kuna bara bara inaingia kulia iache, mbele kidogo kuna barabara nyingine inaingia kulia ukiingia nayo hiyo itakufikisha duka moja maarufu la vioo vya magari linaitwa Limpopo...kabla ya hilo duka hiyo njia itaingia kusho kisha kulia tena basii huo mtaa utaona magari mengi sana yaliyopata ajali na maduka mengi sana ya spea used...hako ndiyo December au chinja chinja...
 
Ukiwa smart na unajiamini trafic wenyewe huwa wana gwaya.. usiwe maneno mengi mengi tu 😀😀Tupo walevi wenye kupenda gari zenye cc kubwa, hiyo inakuwa mteremko kwetu 😃😃
nimeamini jamaa yetu wewe magari mapya ya serikali au Taasisi ndio maana hukamatwi, hakuna Traffic wengi na wabaya km wa Arusha, hata Kangi Lugola alishafumua ngazi ya juu. Hiyo double road wamejaa na Camera ukiingia toa Tengeru wapo pale Chama, km unaelekea Moshi USA river, king'ori kwa Sadala njia ya Machame, Moshi Tech, yaani ni mwendo chini ya 50, au labda tuna magari yenye namba za zamani ndio tunaonewa kila tukitokeza wanajua pesa ya kubrush, Magari ya STK, SU, DFP hamguswi
 
Njia ya Arusha-Moshi kuna sehemu katikati ni pori kuna Kona fulani ila kuna 50kph limit. Sasa porini kuna sababu gani ya kuweka 50kph limit?
 
Nahisi nimeshapia juzi kati hapo.

Si hufiki ile njia ya kuingia stand ndogo?

Nyuma kidogo unaingia kulia?
 
Hiyo double road imekaa kishamba sana.

Highway kubwa hivyo unaweka speed mwisho 50kph?

Morogoro road kuanzia kipande cha kimara na kuendelea watu wanajiachia vilivyo.

Ingekuwa wanaweka mwisho 50kph, wangekula hela nyingi sana.
 
Mkuu situmii STL SU J DFP 😃😃😃... na sijawahi simamishwa.. na hata ikatokea nikasimamishwa sija cha kuhofia nitasimama tu
 
Ushauri muhimu sana huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…