Wazee wa Tec: Hizi All in One PC kuna kitu pale au takataka tu?

Wazee wa Tec: Hizi All in One PC kuna kitu pale au takataka tu?

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Nataka nianze work from home.

Sasa naulizia hizi PC naziona online bei Tsh 550-750k All in One, majina makubwa kama Dell, HP, Lenovo.
Screenshot_20250309-225629.png

Sasa niko hapa najiuliza, zina faa au danganya toto?
Screenshot_20250309-225725.png

Kama aliewahi kutumia matumizi mbalimbali anao mrejesho.
 
Inategemea na mahitaji yako na spec za hizo PC.

Hiyo form factor ya all in one ina advantage na disadvantage advantage rahisi kusetup hakuna box la kuchukua nafasi nyingine hakuna wire kibao za kuunga unga etc. Ukitafuta wireless keyboard/mouse combo unaweza kuchoneka usb dongle moja tu kila kitu kipo connected.

Disadvantage mara nyingi ngumu kufanya upgrades kufananisha na desktop, vitu kama monitor za ziada inabidi uangalie kuna zenye hdmi output na kuna ambazo hazina, kufanya repair au replacement ya parts inaweza ikawa ngumu kupata.

Laptop inaweza ikiwa na advantage zengine hasa portability kasoro monitor ndogo inachosha. Sio lazima mac hiyo dhana potofu tena unaweza ukapata shida kama kazi zako zinahitaji software za windows.
 
Inategemea na generation na matumizi ila kwa sasa PC au laptop nyingi zimekuja na mfumo wa type-c ambao kama utapenda nguvu ya ziada kiutendaji utanunua external GPU au Graphic Card external
IMG_0811.jpeg
IMG_0812.jpeg
 
Computer ni kama gari tu, inategemea unataka kufanyia nini. Huwez beba nondo kwenye harrier. The same to computer.

Vitu vya msingi
1. Processor
2. Battery
3. Graphic card
4. Ram
5. Storage
6. Portability (laptop or desktop)

Hayo yote yatategemea na matumizi yako ndio ujue kipi utakipa kipaumbele.
 
Nataka nianze work from home.

Sasa naulizia hizi PC naziona online bei Tsh 550-750k All in One, majina makubwa kama Dell, HP, Lenovo. View attachment 3265082
Sasa niko hapa najiuliza, zina faa au danganya toto?
View attachment 3265083
Kama aliewahi kutumia matumizi mbalimbali anao mrejesho.
All in one ni laptop tu zilizochangamka na nyingi zipo under speced.

Kama nafasi ni issue nunua mini pc za HP elitedesk (ambazo zinapatikana kirahisi Tanzania) ama Lenovo Thinkstation/Thinkcentre. Unaweka nyuma ya Monitor huwezi ona tofauti na All in one.

images-4.jpeg


Kwa same price ni rahisi zaidi kununua Monitor na mini pc.
 
Back
Top Bottom