X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,400
- 14,339
Mimi ni kijana Ambae Kwa kiasi kikubwa asilimia 75 ya maisha yangu Hadi kufikia hapa nilipo fikia nimelelewa na mababu zangu, na toka enzi hizo Hadi hivi sasa nathamini sana mawazo ya wazee na Huwa nayaenzi Kwa vitendo {alale mahali pema peponi BABU yangu}.
Leo nataka niwape Siri ya ile LAANA waliyokuwa wanaitoa wazee wa zamani Kwa watoto wao ambao walikuwa wanatofautiana nao Kwa itikadi... Siku Moja niliwakuta wazee wawili ambao Kwa bahati mbaya wote hivi sasa ni marehemu {R.I.P} wazee hao walikuwa wanapiga story zao.
Kwakuwa sikujua zilipo anzia nikawa mpenzi msikilizaji, ukizingatia enzi hizo wakubwa wakiongea ilikuwa sio Tabia nzuri kuingilia mazungumzo Yao. Wazee wale walikuwa wanajisifu jinsi walivyo kuwa wana wapa adhabu watoto wao. Mzee mmoja akasema Mimi kijana wangu akinikera TU Huwa nambebesha Dunia azunguke nayo.
Mzee mwingine nae akadakia haki vile hata Mimi ndicho Huwa nakifanya Kwa watoto wangu, akileta ujeuri nambebesha Dunia. Kuna mtoto wangu Fulani, (akamtaja Jina) yule nimembebesha Dunia ataangaika sana ataishia kupata pesa za kula TU.
Kwasababu nilikuwa mtoto sikuelewa maana ya kubebeshwa Dunia.
Miaka kadhaa baadae nilibahatika kufanya mafunzo Fulani yanayoendana na ya kijeshi, kwenye mafunzo hayo ulikuwa ukikutwa na kosa Kuna zoezi unapewa kama adhabu 🤣🤣 kubebeshwa Dunia,
Niliwahi kubahatika kupata hiyo adhabu, haki vile ndani ya dakika kadhaa nikawa napata maumivu kama vile kweli nimeibeba Dunia. Kipindi nipo kwenye hiyo adhabu nikawakumbuka wale wazee waliokuwa wanazungumzia juu ya kuwabebesha Dunia watoto wao. Nikaiambia nafasi yangu kuwa kumbe hivi ndivyo Dunia inavyo bebwa 🤣🤣🤣
Kumbe nilikuwa najidanganya....
Ndugu zangu wazee wa zamani ulikuwa ukiwakwaza wanakulaani Kwa maneno, baada ya hapo wanaingia kilingeni kunena na miungu Yao ya asili, kwenye manuizi Yao hayo ya LAANA Kuna mafundo walikuwa wanayafunga huku wananuia mambo mabaya yakufike. Ndio maana enzi hizo utasikia huyu mama yake anafundo nae.
Mzazi akisha kufungia utahangaika Hadi ukome. Baadae ukikutana na rafiki yake huyo mzazi wako atajidai kukushauri ukamuombe msamaha mzazi wako. Na kweli ukienda kumuomba msamaha. Anafungua fundo mambo yanaanza kukunyookea🤣🤣🤣🤣
Kwa kifupi wazee wa zamani walikuwa wanatupa LAANA na hiyo LAANA wanaisindikizia na kukuLoga🤣🤣🤣🤣
Watu wamelogwa sana Kwa kisingizio Cha LAANA...!