Wazee wacharuka Zanzibar eneo lao ladaiwa kuporwa na watoto wa mstaafu Amani, DC anena mazito

Wazee wacharuka Zanzibar eneo lao ladaiwa kuporwa na watoto wa mstaafu Amani, DC anena mazito

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
11 March 2025
Nungwi Kiungani
Kaskazini Unguja

ARDHI YA MASIKINI WASILAZIMISHWE KUUZA, BALI WAIKODISHE KWA WAWEKEZAJI ILI WAPATE KIPATO ENDELEVU

View: https://m.youtube.com/watch?v=n1wBSC3B3-E

Maoni:
Ardhi ni mtaji wa masikini kwa wazee wenye umiliki wa ardhi maeneo prime (yanayovutia wawekezaji) kama hayo , wapewe elimu na kukingiwa kifua na serikali, ili badala ya kulipwa fidia au kuiuza basi waikodishe wapate kipato milele

Mgogoro wa Ardhi huko Nungwi Kiungani, Wananchi badala ya kuuza ardhi wangewakodisha wawekezaji kwa mfumo wa Nyarubanja. Na wananchi hao kubakia na mtaji wao milele.

Ni wakati muafaka kuurudia mfumo wa Nyarubanja, iwe ardhi iliyopo ufukweni ya wenyeji au mgodi wa dhahabu, madini adimu mkakati, kilimo kikubwa cha miti ya mbao n.k

Wananchi waelimishwe na kupata ushirikiano kutoka serikalini mikataba iwe ya wananchi kukodisha ardhi yao milele kwa wawekezaji wakubwa wakija badala ya kuiuza na kupata kipato cha mkupuo mmoja.

Mfumo huu unatumika hata uarabuni ambapo mgeni ni lazima kuingia ubia na mwenyeji. Mwenyeji ni mwinyi mwenye kipande cha ardhi ambacho ndiyo mtaji wake katika mradi atakao uanzisha mwekezaji iwe hoteli, kisima cha mafuta au ujenzi mkubwa wa kiwanda n.k

Mwekezaji mgeni hutakiwa kumlipa mwenyeji kodi ya kiwanja atakakacho tumia mwekezaji huku mwenyeji au familia ya mwenyeji wakiendelea kuwa na hati miliki ya kiwanja milele na kuilipa serikali kiasi kidogo kama kodi ya ardhi. Watanganyika na wazanzibari waamshwe na kuungwa mkono kwenye suala hili badala ya kufukuzwa, kulipwa fidia au kuhamishwa bali wasapotiwe kuingia mikataba ya kuwapatia mapato milele

Muonekano wa eneo la Nungwi Zanzibar katika picha (chini). Ni Fursa, Eneo la wananchi kupata mapato milele na kuilipa serikali kodi baada ya ardhi yao kukodishwa na mwekezaji
1741743012940.jpeg

Nyarubanja system. In this form of feudalism the major means of production was land. Under Nyarubanja system in Buhaya and Karagwe there was two classes, that is the Batwazi (ruler) and Batwana (serfs). These two classes had to pay rent in kind and rent in labour services to the land lords.

READ MORE :
FEUDAL MODE OF PRODUCTION (FEUDALISM).
The term feudalism originated from the Germany word “feud” which means fees. In this context fees refer to payment of tax.
Feudalism; was the third mode of production and second pre-capitalist mode of production based on exploitation of man by man. The economy of feudal society was based on private ownership and renting of land and livestock by the ruling classes.

CHARACTERISTICS OF FEUDALISM
1. Agriculture became the major economic activity: Following the discovery of iron technology productive forces were improved drastically.

2. Payment of rent to the land lords; rent was paid in various forms.
Labour rent; existed in form of labour or service in which peasants (serf) were required to work for three days in week for the land lords.
Rent in kind: The serfs regularly had to deliver the quantities of his products to the land lords. The products could be in form of grain, cattle or vegetables.
Money rent: Was the system in which money used as a major means of paying rent.
3. Exploitation of man by man example peasants (serf) were exploited by land lords and the distribution of production was not equal.
4. Little freedom to peasant; peasants were tired due to various restrictions as they were treated as children.
5. Private ownership of major means of production such as land, mining sites, houses and cattle all these belonged to feudal lords.
6. Division labour This based on age and sex where men specialized in military while women specialized in farming and taking care of children.
7. Existence of classes; landlords as exploiters and serfs as exploited class.
8. Little surplus enjoyed by feudal lords.

9. Existence of strong political institutions in form of kingdoms and empires example Bunyoro, Buganda and Karagwe. Feudalism in Africa existed in various forms. Its nature depended on place in which it was practiced for instance societies that exercised feudalism were those found in the interlacustine region of East Africa, South Africa, West Africa and the North Eastern Africa.
10. Improved productive forces:Especially tools applied in agriculture and military warfare, this was brought about by iron technology. Generally, African kingdoms such as Buganda and some forest states of West Africa, used means of production centered around either land or livestock-especially cattle-peasants could use the land freely but they were required to pay rent.
FEUDAL RELATIONS/FORMS OF FEUDALISM
1. Nyarubanja system.
In this form of feudalism the major means of production was land. Under Nyarubanja system in Buhaya and Karagwe there was two classes, that is the Batwazi (ruler) and Batwana (serfs). These two classes had to pay rent in kind and rent in labour services to the land lords.
In Buganda Nyarubanja system known as Mvunjo and Busulo, there were two classes that is Bataka (chiefs) and the poor people who rendered labour service and paid of their products to the land lords known as Bakopi. Under the system labour services provider was known as Akasamvu and part of their products was provided to the ruling class known as Obusulu. Bunyoro was the kingdom practiced feudalism in East Africa. The kingdom was divided into provinces known as Saza’s under chiefs. Also there was caste system in East Africa under this feudal system there was two classes which were Bahima (pastoralists) and Bairu (agriculturalists). Bahima who were pastoralists dominated and employed the Bairu who were agriculturalists. It was common in Rwanda, Burundi and Buhaya.

2. Umwinyi system was another form of feudalism found along the coast of East Africa. Wamwinyi controlled the productive forces such as land, serfs and tenants; also monopolized the political and economic power. The serfs and tenants were given land by Wamwinyi (feudal lords) to live on them in return of labour services and tributes which were paid to Wamwinyi. Before Arabs colonization The Mwinyi mkuu was the greatest land lords and ruled Zanzibar with the help of Shehe in Unguja and Diwani in Pemba.

3. Ubugabire system was another form of feudalism practiced among the Tutsi and Hutu in Rwanda and Burundi. The Tutsi (donor) also known as SEBUJA could transfer their cattle to the Ifutu (recipient) as sometimes known as BUGABIRE. The Omugabire and his family were obliged to perform several duties for the masters including house building cultivating.

4. Ntemi system: This was practiced among the Nyamwezi and Sukuma. The power of ruler was based on the control of land The Mtemi organized his people to open up new land wherever it was available. The process of opening up new land was known as Kutema.

MERITS OF FEUDALISM
The following are some of merits of feudalism;
1) The weaker people in the society were protected by the king or the rich land owners. For example, among the Rwandans, the Tutsi had an obligation to protect their tenants, the Hutu.
2) The land owners gave all poor people in the society a piece of land to cultivate. This way, everyone had a means of earning a living.
3) There was a piece in the state as the rich classes maintained law and order.
4) The rich supported the poor with food during drought and famine.
5) The society were highly stratified, with each class of people knowing their position and role. In this way, the feudal societies were very organized. ...... Read more source : Feudalism
 
TOKA MAKTABA 2021
Waziri akosea kubeza mfumo wa Nyarubanja kwa wananchi walio na ardhi. Mfumo wa Nyarubanja ukitumika vizuri utafanya wananchi wenye ardhi kuingiza kipato kutokana na ardhi wanayomiliki pia kuweza kulipa kodi serikalini na katika halmashauri.

Ardhi ni mtaji, Ardhi ni utajiri, Ardhi ni Kipato kama biashara nyingine yoyote. Ardhi inaleta shughuli ya kiuchumi au kwa maneno mengine ajira. Serikali ielimishwe kuwafanya wananchi wawe tajiri kupitia ardhi wanayo imiliki.

Hata National Housing, NSSF, Serikali inapoanzisha miradi badala ya kulipa fidia au kunyakua ardhi wawe wanawaunganisha wenye ardhi wanyonge kwa kuwalipa mapato kila mwezi au kila mwaka milele kwa kuwa wananchi mtaji wao ni ardhi waliyonayo.

TOKA MAKTABA:

03 June 2021
WAZIRI LUKUVI AVIMBA TUNAJENGA ELFU MOJA - "HATUTAKI NYARUBANJA HAPA"

Waziri Wa Ardhi William Lukuvi Amesema Shirika La Nyumba La Taifa linajenga Nyumba Elf Moja Jijini Dodoma Lengo Kuu Likiwa Ni Kuuza Lakini Mradi Huu Wa Ujenzi Ni Shamba Darasa Kwa Wakandarasi Wa Ujenzi Wa Nyumba Za Kuuza

View: https://m.youtube.com/watch?v=1WvDIB5y8o8

Mradi wa NSSF Kigamboni Dar es Salaam Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=xFNA6FVZPlY
 
Yamepangwa vizuri kama GAZA vile, lakini mbona hawayamalizii au ndio wameshapiga sasa wameshindwa kumaliza mradi?
 
11 March 2025
Nungwi Kiungani
Kaskazini Unguja

ARDHI YA MASIKINI WASILAZIMISHWE KUUZA, BALI WAIKODISHE KWA WAWEKEZAJI ILI WAPATE KIPATO ENDELEVU

View: https://m.youtube.com/watch?v=n1wBSC3B3-E

Maoni:
Ardhi ni mtaji wa masikini kwa wazee wenye umiliki wa ardhi maeneo prime (yanayovutia wawekezaji) kama hayo , wapewe elimu na kukingiwa kifua na serikali, ili badala ya kulipwa fidia au kuiuza basi waikodishe wapate kipato milele

Mgogoro wa Ardhi huko Nungwi Kiungani, Wananchi badala ya kuuza ardhi wangewakodisha wawekezaji kwa mfumo wa Nyarubanja. Na wananchi hao kubakia na mtaji wao milele.

Ni wakati muafaka kuurudia mfumo wa Nyarubanja, iwe ardhi iliyopo ufukweni ya wenyeji au mgodi wa dhahabu, madini adimu mkakati, kilimo kikubwa cha miti ya mbao n.k

Wananchi waelimishwe na kupata ushirikiano kutoka serikalini mikataba iwe ya wananchi kukodisha ardhi yao milele kwa wawekezaji wakubwa wakija badala ya kuiuza na kupata kipato cha mkupuo mmoja.

Mfumo huu unatumika hata uarabuni ambapo mgeni ni lazima kuingia ubia na mwenyeji. Mwenyeji ni mwinyi mwenye kipande cha ardhi ambacho ndiyo mtaji wake katika mradi atakao uanzisha mwekezaji iwe hoteli, kisima cha mafuta au ujenzi mkubwa wa kiwanda n.k

Mwekezaji mgeni hutakiwa kumlipa mwenyeji kodi ya kiwanja atakakacho tumia mwekezaji huku mwenyeji au familia ya mwenyeji wakiendelea kuwa na hati miliki ya kiwanja milele na kuilipa serikali kiasi kidogo kama kodi ya ardhi. Watanganyika na wazanzibari waamshwe na kuungwa mkono kwenye suala hili badala ya kufukuzwa, kulipwa fidia au kuhamishwa bali wasapotiwe kuingia mikataba ya kuwapatia mapato milele

Muonekano wa eneo la Nungwi Zanzibar katika picha (chini). Ni Fursa, Eneo la wananchi kupata mapato milele na kuilipa serikali kodi baada ya ardhi yao kukodishwa na mwekezaji
View attachment 3267379
Nyarubanja system. In this form of feudalism the major means of production was land. Under Nyarubanja system in Buhaya and Karagwe there was two classes, that is the Batwazi (ruler) and Batwana (serfs). These two classes had to pay rent in kind and rent in labour services to the land lords.

READ MORE :

Hii siyo nchi ya kihaya
 
Hii siyo nchi ya kihaya

Nilikuwa nikisoma hotuba za Nyerere mtandaoni lakini nyingi sikuelewa hadi nilipoona wazee hawa wa Nungwi Zanzibar kuhusu uchumi wanao lakini wanaukalia

Nyerere - "Uchumi mnao ila mnaukalia"​

1741775856610.jpeg

Picha maktaba: Mwl. Nyerere akihutubia.

More info:
MAKALA KUTOKA MAKTABA :
Chanzo: Dira Mei 2014.
Marehemu baba wa taifa mwl Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa Tanzania uchumi tunao ila tunaukalia. Wapo waliomwelewa.

Pia wapo ambao hawakumuelewa kiasi cha kumtafsiri walivyojua na walivyotaka. Habari kuwa Tanzania inapoteza dola za kimarekani bilioni 1.8 kwa mwaka tokana na utawala na usimamizi mbovu wa raslimali za nchi ni ushahid wa usemi huu.

Nia ajabu zilipotangazwa viongozi wetu hawakukereka wala kuona lau aibu. Wameendelea na upuuzi ule ule kudai wapo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wakati ni unafiki mtupu.

Hakuna kuzungusha. Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndiyo imetufikisha hapa. Ajabu wakati ikitusaliti na kutuuza mchana kweupe walevi wake wa madaraka wanapoteza pesa na muda wetu kutwambia nani anafaa kutuongoza kwa kuwakandia wapinzani wakati wa kuambiwa hawafai ni hao hao walimu wetu wa nani atuongoze na mfumo upi ututawale.

Ajabu hawa wanaoshindwa kusimamia raslimali zetu wanajisifia ubingwa wa kuombaomba na kukopa kopa wasijue wanazidi kuzamisha taifa! Wengine wamestaafu na kujiingiza kwenye magendo na uchuuzi.

Sikumbuki kumsikia katibu mkuu wa CCM Abdulrahaman Kinana wala katibu wa uenezi, Nape Nnauye wakiongolea uchafu huu zaidi ya kuendelea na wimbo ule ule wa jogoo. Lau kutokana na chuki za kibinafsi na ukweli wa hali halisi ya mparaganyiko wa serikali Nape amerudia kuwaita wenzake mizigo japo naye ni mzigo huo huo.

Huu ni ushahidi kuwa tusingekuwa na viongozi na watendaji mizigo, kwa raslimali tulizojaliwa Tanzania haipaswi kuwa maskini. Sana sana ilipaswa kushindana na Singapore na Korea ya Kusini nchi ilizokuwa ikizipiku kiuchumi wakati wa kupata uhuru.

Bahati nzuri habari hii ilitoka wakati wa ziara yao mkoani Tabora. Watu wa Tabora walitumia fursa hii kumtumia salamu rais Jakaya Kikwete kupitia kwa Kinana wakitaka atimize ahadi yake ya kujenga bomba la maji toka ziwa Nyanza.

Nadhani wangemwendea angesema hakuna fedha ya kufanya hivyo wakati serikali yake ikisifika kwa upuuzi wa kuacha wageni waje wachote na kwenda kujitajirisha wao na nchi zao wakati watu wetu na taifa letu wakiendelea kutopea kwenye umaskini wa kutengenezwa na watawala wavivu wa kufikiri kama aliyeanzisha msemo huu.

Kujitoa kimasomaso na kukwepa uwajibikaji, Kinana aliwarushia lawama viongozi wa afya akisema, “Viongozi hawa ni wazembe, wamangimeza na warasimu wanaokwamisha maendeleo ya wananchi. Nakwenda kushikana nao mashati ni lazima wasajili zahanati hizo.” Ama kweli nyani haoni nonihino lake!

Kuna wazembe kama viongozi wa juu wa taifa wanaoruhusu uchumi wetu kunufaisha majambazi wa kimataifa wanaoshirikiana nao? Sikutegemea lolote toka kwa Kikwete kwa kujua fika yeye ndiye mzizi wa balaa hili.

Hakuna kilichokera kama kugundua kuwa deni la taifa limeumka huku tukipoteza pesa ambayo ingeweza hata kulilipa tena pesa yenyewe tuliyopoteza ndani ya miaka kumi tu.

Japo Nyerere alisema: Uchumi tunao tumeukalia, unaweza kuongeza: Akili tunazo lakini hatuzitumii na kama tunazitumia basi ni vibaya na mbaya.

Kuna viongozi wababaishaji na wasanii wanaotoa ahadi wasizitekeleze ukiachia mbali wanaodandia mambo ya kuwarushia lawama wengine wakati wa kulaumiwa ni wao kama tulivyoonyesha hapo juu.

Kuna viongozi manunda na manyang’au wenye uroho na roho mbaya. Hata uwaseme vipi wanajifanya hawasikii wala hawaoni na kuendelea na jinai yao ya kuhujumu taifa letu.

Juzi mbunge wa Kigoma Kusini kwa mfano amewatuhumu maafisa wakubwa wa serikali kwa wizi wa shilingi bilioni 200 toka Benki Kuu. Ajabu ya maajabu hakuna anayewashinikiza wawajibishwe na kuchunguzwa hata kuchukuliwa hatua za kisheria.

Nani amwambie nani wakati wote lao ni moja? Ni bahati mbaya kuwa na wananchi wetu nao wamekuwa kama kondoo wanaojirahisi kuelekea machinjioni. Hwafurukuti wala kuonyesha hasira zao.

Imefikia mahali habari kama hizi zenye kuchusha na kukera zinaonekana kama udaku na burudani kwa waathirika maskini wa nchi hii. Uchumi yaani akili wanazo lakini wanaukalia.

Uchumi yaani umoja na nguvu wanavyo lakini wanavikalia huku wakalia kulia na kulalamika bila kuchukua hatua. Wanaliwa lakini hawastuki. Je tatizo ni nini? Woga, au ukosefu wa uaminifu na uzalendo kwa watu binafsi?

Jiulize ni kiasi gani cha madini tunapoteza kila mwaka ukiachia mbali pesa ya kodi ambayo imefikia hizo dola za kimarekani takribani bilioni mbili? Je ni watalii kiasi gani wanaingizwa kinyemela kutokea nchi jirani ukiachia mbali wanyama wanaouawa kwenye ujangili hadi kuweza kusafirishwa wakiwa hai bila mamlaka kufanya lolote?

Tanzania ingekuwa na watu makini na wenye kupenda taifa lao bila shaka serikali ya rais Kikwete ingeishatimuliwa miaka mingi iliyopita. Lakini nani wa kumwajibisha nani iwapo hata watu binafsi hawako tayari kuwajibika kwa nafasi yao kwa kulikomboa taifa lao toka mikononi mwa wababaishaji na matapeli wa kisiasa?

Jiulize taifa linapoteza mabilioni kiasi gani kwa kulipa wafanyakazi hewa, walioghushi wasiofanya kazi bali kubabaisha na matumizi mengi ya kipumbavu kama ilivyogundulika hivi karibuni ambapo tiketi za ndege za wakubwa kwenda kutanulia nje zililanguliwa mara 16 na serikali ikaendelea na wimbo wake wa kuleta maendeleo kwa watanzania? Mnaleta maendeleao au maangamio?

Jiulize ni wahalifu kiasi gani toka Asia na kwingineko wamegeuza Tanzania kichaka cha kufanyia uovu wao. Mmojawapo wa hivi karibuni ni yule anayejidai kununua IPTL wakati ni mwizi wa kawaida.

Imefikia mahali mtu akikutajia jina Tanzania kinachokuja akilini haraka haraka ni utapeli, usanii, uzembe, ubabaishaji na maangamizi ya kujitakia. Kuna kipindi watu walilalamikia ujenzi wa viwanja vya ndege binafsi kwenye machimbo ya madini ambavyo vinatumika kutorosha madini.

Ajabu watanzania wameendelea na mambo yao kama kawaida kana kwamba kadhia hii imeshughulikiwa. Kwa kujua udhaifu wao serikali wala huwa ahangaiki na kutatua kero yoyote zaidi ya kuongeza spidi ya kula na kufanya madudu.

Wakati wa kuwataka watanzania watumie uchumi wao uwe raslimali, akili, urathi wa utulivu na nyingine nyingi kujikomboa badala ya kuendelea kushikwa matekwa na genge la wahalifu ni huu. Hakika, uchumi mnao ila mmeukalia tu.
Chanzo: Dira Mei 2014.
source : Uchumi mnao ila mnaukalia
 
TOKA MAKTABA 2021
Waziri akosea kubeza mfumo wa Nyarubanja kwa wananchi walio na ardhi. Mfumo wa Nyarubanja ukitumika vizuri utafanya wananchi wenye ardhi kuingiza kipato kutokana na ardhi wanayomiliki pia kuweza kulipa kodi serikalini na katika halmashauri.

Ardhi ni mtaji, Ardhi ni utajiri, Ardhi ni Kipato kama biashara nyingine yoyote. Ardhi inaleta shughuli ya kiuchumi au kwa maneno mengine ajira. Serikali ielimishwe kuwafanya wananchi wawe tajiri kupitia ardhi wanayo imiliki.

Hata National Housing, NSSF, Serikali inapoanzisha miradi badala ya kulipa fidia au kunyakua ardhi wawe wanawaunganisha wenye ardhi wanyonge kwa kuwalipa mapato kila mwezi au kila mwaka milele kwa kuwa wananchi mtaji wao ni ardhi waliyonayo.

TOKA MAKTABA:

03 June 2021
WAZIRI LUKUVI AVIMBA TUNAJENGA ELFU MOJA - "HATUTAKI NYARUBANJA HAPA"

Waziri Wa Ardhi William Lukuvi Amesema Shirika La Nyumba La Taifa linajenga Nyumba Elf Moja Jijini Dodoma Lengo Kuu Likiwa Ni Kuuza Lakini Mradi Huu Wa Ujenzi Ni Shamba Darasa Kwa Wakandarasi Wa Ujenzi Wa Nyumba Za Kuuza

View: https://m.youtube.com/watch?v=1WvDIB5y8o8

Mradi wa NSSF Kigamboni Dar es Salaam Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=xFNA6FVZPlY

Eneo halina mwenyewe mwenye uchungu. Kama lingekuwa linamilikiwa kwa njia ya mfumo wa Nyarubanja angeweza kulikodi kwa mtu mwingine kutokana na mwekezaji kushindwa kutimiza malipo kwa mwinyi mnyarubanja aliyekuwa anategemea kupata kipato kutokana na ardhi hiyo ya Kigamboni.
 
Back
Top Bottom