Wazee walioanzisha vuguvugu la kusaka Uhuru

Wazee walioanzisha vuguvugu la kusaka Uhuru

Libya

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2016
Posts
790
Reaction score
1,968
Kutoka kulia waliosimama:

1. Abdallah Shomari (Tandamti no. 3)
2. Nassoro kalumbanya (simba str.)
3. Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo str.)
4. Mtoro Ally (Muhonda str.)
5. John Rupia (Misheni kota)
6. Julius Nyerere( Pugu Sekondari)
7. Said Chaurembo (Congo/ Mkunguni str.)
8. Jumbe Tambaza (Upanga )
9. Sheikh Suleiman Takadir (Mafia /Swahili)
10. Dossa Aziz ( Mbaruku /Somali kipande)
11. Mshume Kiyate (Tandamti)
12. Juma Sultan (Kitchwele karibu na kanisa dogo) 13. Maalim Shubeti (Masasi/ Likoma)
14. Rajab Simba (kiungani str.)
15. Waziri Mtonga (Kilosa no.
18' Ilala)
16. Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
17. Maxi Mbwana (Aggrey /Kongo)
18. Usia Omari (Sungwi, Kisarawe)
19. Sheh Issa Nasir (Bagamoyo)
IMG-20230216-WA0042.jpg
 
Ya nini kitu kwa sasa?! Why should we crack our minds to read this? 50's has gone.
 
Ficha huu uzi Mzee Mohammed said asiuone na hujamtaja sykes😂, nakuchokoza hapa Babu yetu Mohamed Said karibu utoe neno
Ficha huu uzi Mzee Mohammed said asiuone na hujamtaja sykes😂, nakuchokoza hapa Babu yetu Mohamed Said karibu utoe neno
Basi...
Picha hiyo mimi ndiye niliyoiweka mtandaoni hadharani.
Picha hii alinipa Msakala Mohamed Jumbe Tambaza.

Aliyenipeleka nyumbani kwa Msakala ni Abdallah Tambaza.

Picha hiyo ilipigwa mwaka wa 1957 ulipokuja ujumbe wa Kamati ya Udhamini ya Umoja wa Mataifa kusikiliza maoni ya Watanganyika.

Kleist Sykes angekuwa hai asingekosekana kwenye kundi hilo la wazee wa Dar es Salaam.

Kleist alifariki mwaka wa 1949.
 
Ya nini kitu kwa sasa?! Why should we crack our minds to read this? 50's has gone.
Joro...
Ikiwa wewe unaona hapana haja ya kuisoma historia hii kwa kuwa miaka mingi imepita sawa hakuna wa kukulazimisha lazima uisome.

Harvard na Oxford University Press, New York walikusanya waandishi yapata 500 mimi nikiwa mmojawapo kuandika Dictionary of African Biography (DAB).

Kleist Sykes ni mmojawapo wa wazalendo kutoka nchi tofauti za Afrika aliyemo ndani ya DAB.

Kazi hii ilichukua miaka mitatu kukamilika 2008 - 2011.
1676580992420.png
 
Basi...
Picha hiyo mimi ndiye niliyoiweka mtandaoni hadharani.

Picha hii alinipa Msakala Mohamed Jumbe Tambaza.

Aliyenipeleka nyumbani kwa Msakala ni Abdallah Tambaza.

Picha hiyo ilipigwa mwaka wa 1957 ulipokuja ujumbe wa Kamati ya Udhamini ya Umoja wa Mataifa kusikiliza maoni ya Watanganyika.

Kleist Sykes angekuwa hai asingekosekana kwenye kundi hilo la wazee wa Dar es Salaam.

Kleist alifariki mwaka wa 1949.
Ahsante sana Mzee, nina swali hapa, juzi kuna video ya interview moja niliona alifanyiwa Nyerere miaka ya 60 mwanzoni,katika interview ile wazungu wanahoji kwanini anaomba uhuru wakati hatukuwa tayari kujiongoza

Sasa swali langu ni kutaka maoni yako kuhusu hii kauli aliyoambiwa Nyetere,je unaona tulipopata uhuru tulikuwa tayari kujiongoza ? ,Hasa ukijaribu kulinganisha hatua ya maendeleo wakati wa Nyerere, alikuwa kiongozi sahihi kuongoza Tanganyika ?,huwa najaribu ku imagine kama nchi angepewa mwingine tungekuwa hatua gani ya maendeleo leo hii.
 
Si kwamba walitoka msikitini?
Tuta...
Haifai ndugu yangu kukejeli dini ya nduguzo.

Nakuwekea vipi babu zangu walivyokuwa waungwana.

Hata siku moja hawakumnyanyapaa Nyerere kwa sababu ya imani yake.
Msikiti una uhusiano gani na picha hiyo ndugu yangu?

Soma hapo chini:

Safari ya Julius Nyerere Lindi 1955

'Lindi ulikuwa mji wa Waislam.

Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwa akishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa.

Watu wachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindi kutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali.

Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wa mjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa na haja ya kuhudhuria ibada pale kanisani.

Hakuna mtu katika uongozi wa TANU wa Lindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote kati yao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale.

Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikiza Nyerere kanisani ili kumpa ulinzi.

Baada ya kujadili suala hilo kwa urefu hatimaye iliamuliwa kuwa Mpunga na wanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize Nyerere kanisani na wengine wabakie nje kulinda mlango.

Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani ya kanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwa na Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu.

Misa hii ‘’maalum’’ ilidumu katika fikra za wale Wakristo waliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sana Wakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi.''

(Kutoka kitabu cha maisha ya Abdul Sykes)

Ndugu zangu wazalendo hawa ni wa kupigiwa mfano si wa kukejeliwa.

1676581577981.jpeg

Salum Mpunga​
 
Ahsante sana Mzee, nina swali hapa, juzi kuna video ya interview moja niliona alifanyiwa Nyerere miaka ya 60 mwanzoni,katika interview ile wazungu wanahoji kwanini anaomba uhuru wakati hatukuwa tayari kujiongoza

Sasa swali langu ni kutaka maoni yako kuhusu hii kauli aliyoambiwa Nyetere,je unaona tulipopata uhuru tulikuwa tayari kujiongoza ? ,Hasa ukijaribu kulinganisha hatua ya maendeleo wakati wa Nyerere, alikuwa kiongozi sahihi kuongoza Tanganyika ?,huwa najaribu ku imagine kama nchi angepewa mwingine tungekuwa hatua gani ya maendeleo leo hii.
Basi...
Sina jibu.
 
Naweka siti hapa, nitachangia kesho leo nina majukumu ya ujenzi wa Taifa.
 
sykes na uhuru wa Tanganyika ni sawa na Yai na Kuku.

Mzee Mohamed Said akisoma uzi wako utakuwa bali kwasababu jina la Babu yake ukiliweka.
Ngongo,
Hiyo ni picha ya TANU 1957.

African Association iliasisiwa 1929 na waasisi wake ni hawa: Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Suleiman Majisu, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Rawson Watts na Raikes Kusi.

Picha ya waasisi hawa ya 1929 haipo lakini ipo picha ya 1933 ya ufunguzi wa jengo la African Association Kleist Sykes yuko pamoja na wazalendo wengine kama Ramadhani Mashado Plantan na Mdachi Shariff.

Hii picha ipo katika kitabu cha Abdul Sykes.

Katika picha hiyo yupo Gavana Donald Cameron na ndiye alifungua jengo hili Mtaa wa New Street na Kariakoo hapo leo ilipo ofisi ya CCM.

Ukitaka kuandika historia ya CCM inakubidi uanze 1929 kama unavyoziona hizo picha hapo chini.

1676606330744.jpeg

Ofisi ya African Association 1933

1676606556498.jpeg

Ofisi ya TANU 1955
1676606415488.jpeg

TANU 1954

Pb0MJ9TRpjeGTK6HAqc4VUE1Qou4XNOfZgDFK59LSAMh_LqUFiB41cwxR37bY6FY1T1INbpLsh4-fsy8V1a0ICrXd1fz-uzbl480wzhqC9Peo7R3i2fZtyb3jZouOKlVkhUgMYOXHc_lJXgiznnk0CbAu4R9hZmlQoq43DLd8RNC5kxxcAeENb31tGlG5Kpy6EjJl-ky1_9DsdPuRrFKunltgzWhOX_9SaPINxMn67gpoQyG19-5_Mc4hTFVkNkbrongmb3k7PqQnR841yOypcca5p_uzbGWnqInAdZbi9gxiFlJR388m2C31H1zgXKooqf9lH2cGFSzy5BNGQjXHUwS6piijnfleZJqxclm3Iwfql_OqkGM1A7GZVV8SuDtXqJ1vBiGAK9uP8-Rpf_5M2_lMU-SXEhOXx64oQ1KvWiPpWt7_Q-VEEb5WaYt_WrhxrPADFmEIkYOFSqOD3MB1gw8cGFIaBnbdivBD_DUJmCRTt6kMZEEUAg0UabO_W4HnQfb2kwtChnclPQCqKJ-saFdQqDVtWQVawWDGycI7oR2OR5k0UGljr39SnobdrzEoRTWkqIlhx4IOgAGsoRfdmrypfp6-0FS340DGQVsHf6aut-D6uBfCWJ5wXSuj4T1FubzhYJl0v8K1rBBh3nvjxRbArziuLoiWPi41NcK_qvg6HSpVPgwQnatvMuCDx0ALTYZfP9kSl-UVubXTcxfl31DUTM7i5vZSGguhV7R5B-XMhXGmwCpzYj93MU20RHKImw5JF3XlEEB1_SFpJDwouZJ-yMpIYcNwgjB3uMEuU60t4HSA6j8sxzTAnXSdd9EYg9xSkIwJh5E5w0SyEC5S5feNcosgWcDjcWezepSczCxvQ_ZvdfgpXPZGp3GcDtt3IJ8EFWR7Dg3rmLQK03aPM0qwyPmzqOxUb82QCEMK4FfZmSbRVrkmcT_vFnN4FfxeexFKRmMbo5fUT4EAD4=w473-h650-no

240863733_1014054866008558_3271995931862167895_n.jpg

Ofisi Ndogo ya CCM​
 
Basi...
Picha hiyo mimi ndiye niliyoiweka mtandaoni hadharani.

Picha hii alinipa Msakala Mohamed Jumbe Tambaza.

Aliyenipeleka nyumbani kwa Msakala ni Abdallah Tambaza.

Picha hiyo ilipigwa mwaka wa 1957 ulipokuja ujumbe wa Kamati ya Udhamini ya Umoja wa Mataifa kusikiliza maoni ya Watanganyika.

Kleist Sykes angekuwa hai asingekosekana kwenye kundi hilo la wazee wa Dar es Salaam.

Kleist alifariki mwaka wa 1949.
Basi...
Ningependa kukufahamisha kuwa hapa JF mimi si babu wa yeyote yule kuwa naweza nikataniwa.

Kwa umri wangu unokimbilia miaka 71 kwenu nyinyi mimi ni baba yenu kwani naamini ni makamo ya mama na baba zenu.

Hii kwangu mimi na kwa wengi ambao babu na baba zetu ndiyo walioanzisha vuguvugu la kupigania uhuru hili si jambo la utani.

Waliotaka kufuta historia hii wao waliona uzito wa jambo hili na hawakulifanyia maskhara.

Walitumia nguvu zao kuhakikisha kuwa historia ya TANU inapotea.

Ingieni kwenye mjadala na mimi kwa staha na heshima zenu kamili.
 
Waungwana wanazidi kupungua kila uchao, machawa na brainless population ndo wanaimiliki dunia kwa sasa
 
Dunia ya sasa fanya mambo yako uende zako na usitarajie mtu mwingine akukumbuke.
Fanya wajibu wako uende zako dunia inaendelea.
Ukikaa kusubiri fadhila utapata magonjwa yasiyotibika.

Ilifika wakati Wazungu waliamua kutupatia Uhuru na sio juhudi zetu.

Wazungu wangependa wangetutawala hadi sasa hivi na hatuna uwezo wa kushindana nao.

Hao Wazee hata wasinge kuwepo uhuru ungepatikana tu.
 
Che...
Sisi tumeandika historia ya wazee wetu sababu kuu ni kule kuona historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika imegeuzwa kuwa historia ya Julius Nyerere peke yake.

Kama nisingeandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes historia hii ingepotea.

Hii mosi kuwa Tanganyika ingepata uhuru bila ya harakati za kudai uhuru hiyo si kweli.

Mimi babu yangu Salum Abdallah aliongoza migomo mitatu mikuu - 1947, 1949 na 1960 kupigania haki za Mwafrika.

Matokeo ya migomo yote hii ni kuongezeka kwa nguvu ya Waafrika kudai nchi yao.

Mgomo wa Tanganyika Railways wa 1960 ulidumu siku 82 na kila kitu kilisimama, mabasi, meli na treni.

Muhimu ni kuijua historia ya uhuru na yote yatakuwa wazi mbele yako.
 
Kutoka kulia waliosimama:

1. Abdallah Shomari (Tandamti no. 3)
2. Nassoro kalumbanya (simba str.)
3. Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo str.)
4. Mtoro Ally (Muhonda str.)
5. John Rupia (Misheni kota)
6. Julius Nyerere( Pugu Sekondari)
7. Said Chaurembo (Congo/ Mkunguni str.)
8. Jumbe Tambaza (Upanga )
9. Sheikh Suleiman Takadir (Mafia /Swahili)
10. Dossa Aziz ( Mbaruku /Somali kipande)
11. Mshume Kiyate (Tandamti)
12. Juma Sultan (Kitchwele karibu na kanisa dogo) 13. Maalim Shubeti (Masasi/ Likoma)
14. Rajab Simba (kiungani str.)
15. Waziri Mtonga (Kilosa no.
18' Ilala)
16. Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
17. Maxi Mbwana (Aggrey /Kongo)
18. Usia Omari (Sungwi, Kisarawe)
19. Sheh Issa Nasir (Bagamoyo)View attachment 2519748
Ukimtoa John rupia na nyerere, wakristo wengine walikua wapi..?
 
Ukimtoa John rupia na nyerere, wakristo wengine walikua wapi..?
Mwalimu...
Katika mswada wa kitabu cha kumbukumbu za Kleist Sykes alioandika kabla ya kifo chake mwaka wa 1949 Kleist anasema viongozi wa kanisa wakiwaonya waumini wao kutojihusisha na siasa.

Mswada huu ni sura katika kitabu alichohariri John Illife, "Modern Tanzanians," (1973).

1677165307446.jpeg

Back
Top Bottom