Wazee wameniomba nigombee!

Mlenge

R I P
Joined
Oct 31, 2006
Posts
2,125
Reaction score
2,306
Masihara pembeni, na mimi wazee wamenishauri nigombee ubunge!

(Jamani hakuna hata mtu mmoja anayesema 'nimeamua mwenyewe kugombea' kuwa Mbunge?)

Lakini mpaka tunaenda mitamboni, sitagombea ubunge mwaka huu!

Mlenge
 
Mimi vijana wamenionya nisigombee ubunge kwani maisha yangu yatakuwa hatarini!
 
mbona hujaweka profile yako sisi tuseme nini Mlenge ?
kama wazee wamekutuma nenda tu
 
Masihara pembeni, na mimi wazee wamenishauri nigombee ubunge!

(Jamani hakuna hata mtu mmoja anayesema 'nimeamua mwenyewe kugombea' kuwa Mbunge?)

Lakini mpaka tunaenda mitamboni, sitagombea ubunge mwaka huu!

Mlenge

Mlenge tupe Cv yako na unataka kugombea wapi?? Kweni wewe una nia ya kugombea sio unasukumwa na wazee!!
 
We uoni watu wanavyopoteza maisha kule bungeni?Amina,Wangwe,Kabuye,MD wa Business Times n.k

na si kupitia bunge tu ndo unaweza kuwa wa manufaa kw ataifa hili, kuna maeneo mengine pia mtu unaweza kuchangia maendeleo ya taifa hili........siasa siasa siasa......
 
Mimi nilitaka kugombea mwaka huu, mzee Mh. Mbunge anayeshikilia jimbo ameniambia nisubiri kidogo, ataniachia mwaka 2015 !!
 
Kabla hujagombea ni lazima uwe na waganga wa kienyeji si chini ya watano.
Maana kuna watu wanatisha kwa mambo flani kule mjengoni.
 
Masihara pembeni, na mimi wazee wamenishauri nigombee ubunge!

(Jamani hakuna hata mtu mmoja anayesema 'nimeamua mwenyewe kugombea' kuwa Mbunge?)

Lakini mpaka tunaenda mitamboni, sitagombea ubunge mwaka huu!

Mlenge
Mlenge,

Mbona wengine kule Kyela tumesema kwamba tumeamua wenyewe bila kufuatwa na wazee au wajukuu?

Lakini bahati mbaya kuna watu hawaamini mpaka useme umetumwa na mtu.
 
Masihara pembeni, na mimi wazee wamenishauri nigombee ubunge!

(Jamani hakuna hata mtu mmoja anayesema 'nimeamua mwenyewe kugombea' kuwa Mbunge?)

Lakini mpaka tunaenda mitamboni, sitagombea ubunge mwaka huu!

Mlenge

Ni kutaka public sympathy ya wananchi tu kutoka kwa wanasiasa uchwara hawa.
Hakuna lolote
 
ili uwe karibu zaidi na wanachi na kama una nia ya dhati na uzalendo wa kweli anza na UDIWANI. uskimbilie UBUNGE

teh teh teh patamu hapo !!!!!!
 
ili uwe karibu zaidi na wanachi na kama una nia ya dhati na uzalendo wa kweli anza na UDIWANI. uskimbilie UBUNGE

teh teh teh patamu hapo !!!!!!

Uko sahihi sana.
Wengi tunawazia ubunge ilhali kuna steji nzuri ya kuanzia.
 
Mimi nilitaka kugombea mwaka huu, mzee Mh. Mbunge anayeshikilia jimbo ameniambia nisubiri kidogo, ataniachia mwaka 2015 !!
Kumbe ni kuachiana na wewe mwaka 2020 utamwachia nani
 
hehe wapo wengi sana wanaenda na gia hiyo.....kuna wenzetu wanadiliki hata kusema wametumwa na raisi....kweli 2010 ipo kazi.....na hili la sheria ya gharama za uchaguzi....!!!
 
sijasikia mgombea anayesema vijana wamemuomba agombee...yani kila mgombea anakuja na wimbo uleule wa kuombwa na wazee..mmmh
 
Hivi watu hawaruhusiwi kufa eeh na wakifa wamerogwa?Yaani tunampangia mungu nafasi yake sio?Wote waliugua, tena magonjwa ya maana kabisa na miili yao iliposhindwa kuendelea kuugua na kuishi roho zilizrudi kwa yule aliyeziumba sasa tusisingizie shida ya kuroga.;Sema hatuwezi kuwajibika tukipatiwa nafasi ya kuwa wabunge tutakuwa kama hao wengine wanaosababisha midomo yao kuvunda. Mlenge nenda kama unataka lakini si kwa kuombwa na wazee. nenda kalete tofauti kama unaamini utaleta.
 
Katika harakati za kusaka ubunge katika jimbo la Hai (CCM) mkoa wa Kilimanjaro, huyu bwana amejichimbia jimboni akitoa misaada mbalimbali. Kama kuna mwenye information za kutosha za huyu bwana kama anafaa kupewa uongozi atujuze tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…