Wazee wanasema

Wazee wanasema

Street brain

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2022
Posts
584
Reaction score
767
Wazee wanasema, "chui akijilamba, huwa analamba rangi za doti zake zote, hachagui chache"🐆. Mwanadamu amekuwa na ubaguzi, wakuchagua watu wake wakuwabembeleza, wakuwafichia siri, kuwadekeza.

Kosa alilotenda anayependwa litaonekana kama wala sio kitu, ila akilitenda mwingine anashukiwa kama radi. Tumejichagulia malaika wetu na kuwabatiza wengine mashetani!

Wanaoitwa mashetani pengine ndio wapambanaji kweli ila hawaonekani! Walishatengwa hata wajitutumue vipi, hawaonekani.

Hawa malaika hata akikohoa tuu, sijui mafua, tayari ameshakimbizwa hospitali! Wale mashetani imebidi watembee na dawa tu, wakikosa kazini watasulubishwa haswa, imebidi wajikaze tuu, kuepusha fujo! ©️Pocco, Katibu wa ndege amewaandikia barua ndege wote watumie midomo vizuri wasidonoe wenzao.😅🙏🏾
 
Yesu mwenyewe alichagua mitume Sasa sembuse sisi lazima uwe na mipaka ...chukua hiyo
 
Dah, maana kuna midomo mingine imechongoka balaaa!
 
Back
Top Bottom