Wazee wenzangu wa Martial Arts Special Thread

Wazee wenzangu wa Martial Arts Special Thread

Huu mchezo hauna kata za hatari ndio maana nimesema hivyo mtaalam... Hata mapigo yake sio deadly na ukikutana na mtu alie master boxing vizuri anakuondoa.
Mkuu elewa kuwa boxing hasa kick box ni nzuri na ni simple sana lakini kama unavyosema kuwa aliecheza shotokan anaweza kupigika, lakini pia inategemea na ujuzi wa mhusika. Kick boxing is simple to practice and more successful compared to other martial arts as it is a hybrid of them. Lakini stance za kick box zinaanzia kulia
 
Nimejaribu sana kutafuta dojo ya jiujitsu lakini sija pata bahati kwa hapa Dar. Nilienda mpaka ubalozi wa Brazil labda watuunganishe na Master wa Brazilian Jiujitsu lakini sikufanikiwa. Jiujitsu origin yake ni Japan lakini napenda ile ya Brazil. Sijui kuna anaye jua wapi wanafundisha kwa hapa Dar?
 
Nimejaribu sana kutafuta dojo ya jiujitsu lakini sija pata bahati kwa hapa Dar. Nilienda mpaka ubalozi wa Brazil labda watuunganishe na Master wa Brazilian Jiujitsu lakini sikufanikiwa. Jiujitsu origin yake ni Japan lakini napenda ile ya Brazil. Sijui kuna anaye jua wapi wanafundisha kwa hapa Dar?
Unataka kwaajili ya sports au self defense? Jiujitsu zinafanana sana na judo, lakini kwanini uhangaike kutafuta waBrazil wakati martial arts zipo nyingi na ziko poa tu kwa ajili ya self defense na sports?
 
Watu wanachanganya kuhusu hizi martial arts, ieleweke tu kuwa kila aina ya martial arts ni nzuri ikiwa tu mhusika atafuata na kuifanya kuwa sehemu ya maisha yake.
Pia ni vema kufahamu tu kuwa kuna ngumi/martial arts za kawaida ambazo raia wote wanaruksa ya kujifunza au kucheza kama self defense na sports mfano wa hizo ni
1.karate
2.taekwondo
3 . kick boxing
4.judo
N.k.
Hizo ni baadhi tu ya sport martial arts kwa wote japo zipo nyingi,
Lakini kuna nyingine ni kwa ajili ya mapigano ya kijeshi (kombat martial arts) mfano ni:-
1 . kombat karate.
2. Judo kombat
3. Krav maga n.k
Hizi ni za kupiga na kuua na haziruhusiwi kufundishwa uraiani bali ni kwa maaskari tu,
Mfano TPDF (hasa commando unit) iko advanced zaidi kwa hapa Tanzania, pia polisi baadhi hupewa mafunzo hayo hasa wale police special forces (red Barret) na si wote,
NB: ujuzi wa ngumi sio tu kujifunza bali pia utayari wa mhusika na utulivu kifkra, unaweza ukafuzu vizuri lakini bila ujasiri na utulivu utapigika.
Aisee kumbe nilibahatika sana kufundishwa KARATE KOMBAT na JUDO KOMBAT, pia hata Master aliyekua ananifundisha alinionya kabisa kwamba, "HII NI MICHEZO YA KIJESHI USITHUBUTU KUPIGANA HOVYO"
Tangu siku hiyo nimekua mwoga sana kupigana na mtu asiepitia Martial Arts,
Ila nashukuru jamaa alinipa na ABC za Boxer maana alishaisoma Saikolojia yangu

ALIAMUA KUNIFUNDISHA KARATE KOMBAT NA JUDO KOMBAT BAADA YA KUONA SHOTOKAN SIILEWI
Ila aliponifundisha KOMBAT akaona ni mwepesi sana wa kushambulia na kutoka
 
MMA imedhihirisha kuwa katika kupigana hakuna formula ni suala la timing tu. Kwa mnaofuatilia UFC mtaona watu wenye backgroung za ujuzi wa michezo mbalimbali ya mapigano wanavyokalishwa kiulainiii...
 
Back
Top Bottom