Wazee wote wapewe pensheni

Wazee wote wapewe pensheni

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,136
Reaction score
32,268
Hello JF,

Leo nimejikuta nafikiria uzee na changamoto zake, hasa kwa wazee waliokua nje ya mfumo wa ajira rasmi kama mafundi, housegirls/ boys, wafanyabiashara ndogo ndogo n.k ni sehemu ningependa kuchunguza wanaishije katika uzee especially wale wa Dar es Salaam na Miji mingine mikubwa ambao labda movements zimewafanya watengane na familia/koo zao?

Mimi ningependa kuona kila mzee anapata basic pension sababu hata wao, japokua hawatambuliki rasmi ila huduma zao ziliweza kusaidia formal sector kuwa kama hivyo ilivyo, mfano housegirls kutunza nyumba na familia wamesaidia baba na mama mwenye nyumba kwenda kazini 🤣🤣🤣😊😊😊😊😊😊 , wafanya biashara ndogo ndogo wanasaidia mzunguko wa pesa mtaani n.k, wale wanaofanya kazi kwenye Ajira rasmi,wanategemea sana wale ambao hawako kwenye ajira rasmi/ informal sector,hivyo WOTE wapewe pensheni, sema wale waliofanya kazi na ku contribute wapewe extra for their services.

Mnaonaje?
 
Mawazo mazuri Sana Tena Sana. Lakini nadhani ni changamoto kwa nchi zetu hizi ambazo bado Ni maskini kuweza kuwawezesha wananchi wake kiuchumi. Na kwa bahati mbaya Sana serikali bado haijaweka vipao mbele maswala Kama haya na Ni vile tu wanajijali wao tu!

Muhimu Mimi nadhani elimu au maarifa yaongezwe hao ulio waainisha hapa waweze Kuweka akiba ili uzee utakapo wawasilia waweze kuustahimili.

Najaribu kufikiria Mimi Kama Mimi Fundi niliejiaji ipo siku sitakua na nguvu ya kufanya kazi na hata ufanisi utapungua halafu mpaka Sasa sijajiandaa kwa Hilo Hali muda unaenda Sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mawazo mazuri Sana Tena Sana.
Lakini nadhani Ni changamoto kwa nchi zetu hizi ambazo bado Ni maskini kuweza kuwawezesha wananchi wake kiuchumi...
Asante mkuu kwa mchango murua lakini hili jambo hata nchi maskini zinaweza, ni kukosa priority kwa serikali zetu tu, mfano kumsomesha kijana kwa miaka mitatu (3), na asipate Ajira huoni ni kutumia vibaya rasilimali zetu?

Pesa ikisimamiwa vizuri hata makundi yaliyosahaulika kama hawa wazee yanaweza kupata msaada
 
Asante mkuu kwa mchango murua,lakini hili jambo hata nchi maskini zinaweza, ni kukosa priority kwa serikali zetu tu, mfano kumsomesha kijana kwa miaka mitatu (3), na asipate Ajira huoni ni kutumia vibaya rasilimali zetu? Pesa ikisimamiwa vizuri hata makundi yaliyosahaulika kama hawa wazee yanaweza kupata msaada
Ni kweli sehemu nyingi Sana serikali inapoteza pesa kwa kiasi kikubwa, ukifuatilia bajeti za serikali zetu Ni moja kwa moja hazina Nia ya kumuinua mtu wa Hali ya chini kuja juu.

Asilimia kubwa utakuta wanafanya kila liwezekanalo waonuke wao na familia zao Kisha vitu vidogo vya kuwadanganyia wapiga kura biashara imeisha.

Uwezo mkubwa serikali ilikua nao wa kuwahudumia watu wazee ambao walilijenga taifa hili kwa namna moja ama nyingine ambao leo hawana nguvu Tena ya kujipatia riziki kwa sababu shuguli zao wakati walipokua Wana nguvu walikua nje ya mfumo unawezesha wao kuja kunufaika uzee kwao, lakini hao serikali haioni kujali!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasipewe pensheni kama hela hakuna
Ila wapewe card zenye exemption ya nauli za mabasi na wapewe insurance ya matibabu wote...

Binafsi .. nafikiri makundi haya yanatakiwa kupewa posho
1.walemavu
2.wajane.
3.wazee
4.waliopoteza kazi
5.wasichana wasio na kazi..
 
Wasipewe pensheni kama hela hakuna
Ila wapewe card zenye exemption ya nauli za mabasi na wapewe insurance ya matibabu wote....
Nimependa Wazo lako , kuna mahali/nchi wanatoa vouchers za matibabu, usafiri na chakula,kwa wazee,, mimi naamini inawezekana
 
Ni kweli sehemu nyingi Sana serikali inapoteza pesa kwa kiasi kikubwa, ukifuatilia bajeti za serikali zetu Ni moja kwa moja hazina Nia ya kumuinua mtu wa Hali ya chini kuja juu.

Asilimia kubwa utakuta wanafanya kila liwezekanalo waonuke wao na familia zao Kisha vitu vidogo vya kuwadanganyia wapiga kura biashara imeisha.

Uwezo mkubwa serikali ilikua nao wa kuwahudumia watu wazee ambao walilijenga taifa hili kwa namna moja ama nyingine ambao leo hawana nguvu Tena ya kujipatia riziki kwa sababu shuguli zao wakati walipokua Wana nguvu walikua nje ya mfumo unawezesha wao kuja kunufaika uzee kwao, lakini hao serikali haioni kujali!

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda Huyu mama tukipiga kelele atatusikia kilio chetu
 
Hello JF,

Leo nimejikuta nafikiria uzee na changamoto zake, hasa kwa wazee waliokua nje ya mfumo wa ajira rasmi kama mafundi, housegirls/ boys, wafanyabiashara ndogo ndogo n.k ni sehemu ningependa kuchunguza wanaishije katika uzee especially wale wa Dar es Salaam na Miji mingine mikubwa ambao labda movements zimewafanya watengane na familia/koo zao?

Mimi ningependa kuona kila mzee anapata basic pension sababu hata wao, japokua hawatambuliki rasmi ila huduma zao ziliweza kusaidia formal sector kuwa kama hivyo, mfano housegirls kutunza nyumba na familia wamesaidia baba na mama mwenye nyumba kwenda kazini [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4] , wafanya biashara ndogo ndogo wanasaidia mzunguko wa pesa mtaani n.k, wale wanaofanya kazi kwenye Ajira rasmi,wanategemea sana wale ambao hawako kwenye ajira rasmi/ informal sector,hivyo WOTE wapewe pensheni, sema wale waliofanya kazi na ku contribute wapewe extra for their services.

Mnaonaje?
Wameifanyia Nini Nchi wengine walikua majambazi wauwaji
 
Wazo jema mkuu, lakini kwa nchi yetu hii... Sina uhakika kama wataliagalia kwa jicho la kuona mbali.
Nchi kama marekani kuna nursing homes za wazee, na na wanaangaliwa na kupewa huduma zote muhimu. Cha msingi ni kuwa na facility ambayo itatoa huduma zote na mahitaji ya msingi (chakula,mavazi, malazi na elimu kwa wahitaji kama watoto wenye umri wa kuwa shule) Vilevile hata kutoa mitaji midogomidogo na ajira ndogondogo kwa watoto wa kike na vijana wa kiume wanaoishi katika mazingira magumu.
 
Mkuu Rebeca 83 I feel like this will make a good idea for a project proposal. Unaweza kuandaa pendekezo lamradi halafu ukatafuta donors na baada ya kupata donors, ukaandaa kitu kama NGO fulani au project fulani special kwa mambo hayo. Halafu ukawa unawapa progress report.
Nakumbuka nikiwa chuo tulijifunza haya mavitu, na nilipata bahati kufanya field katika NGO moja walikuwa wanajishughulisha na kuwawezesha wasichana na wanawake wadogo. Walikuwa wanapokea fedha kutoka kwa donors na walikuwa wanafanya evaluation na kutuma evaluation report kila baada ya miezi mitatu, ambayo ndiyo kipindi cha kutoa elimu, mitaji midogomisogo na mafunzo kwa walengwa wa mradi.
 
Asante rafiki kwa mawazo mazuri
 
Hello JF,

Leo nimejikuta nafikiria uzee na changamoto zake, hasa kwa wazee waliokua nje ya mfumo wa ajira rasmi kama mafundi, housegirls/ boys, wafanyabiashara ndogo ndogo n.k ni sehemu ningependa kuchunguza wanaishije katika uzee especially wale wa Dar es Salaam na Miji mingine mikubwa ambao labda movements zimewafanya watengane na familia/koo zao?

Mimi ningependa kuona kila mzee anapata basic pension sababu hata wao, japokua hawatambuliki rasmi ila huduma zao ziliweza kusaidia formal sector kuwa kama hivyo, mfano housegirls kutunza nyumba na familia wamesaidia baba na mama mwenye nyumba kwenda kazini [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4] , wafanya biashara ndogo ndogo wanasaidia mzunguko wa pesa mtaani n.k, wale wanaofanya kazi kwenye Ajira rasmi,wanategemea sana wale ambao hawako kwenye ajira rasmi/ informal sector,hivyo WOTE wapewe pensheni, sema wale waliofanya kazi na ku contribute wapewe extra for their services.

Mnaonaje?
Watu ambao mna akili ya kuwa viongozi bora mmebaki kuandika JF.
Kongole na Mungu akubariki kwa wazo zuri.
 
Wasipewe pensheni kama hela hakuna
Ila wapewe card zenye exemption ya nauli za mabasi na wapewe insurance ya matibabu wote...

Binafsi .. nafikiri makundi haya yanatakiwa kupewa posho
1.walemavu
2.wajane.
3.wazee
4.waliopoteza kazi
5.wasichana wasio na kazi..
Watu ambao mna akili ya kuwa viongozi bora mmebaki kuandika JF.
Kongole na Mungu akubariki kwa mawazo mazuri.
 
Hello JF,

Leo nimejikuta nafikiria uzee na changamoto zake, hasa kwa wazee waliokua nje ya mfumo wa ajira rasmi kama mafundi, housegirls/ boys, wafanyabiashara ndogo ndogo n.k ni sehemu ningependa kuchunguza wanaishije katika uzee especially wale wa Dar es Salaam na Miji mingine mikubwa ambao labda movements zimewafanya watengane na familia/koo zao?

Mimi ningependa kuona kila mzee anapata basic pension sababu hata wao, japokua hawatambuliki rasmi ila huduma zao ziliweza kusaidia formal sector kuwa kama hivyo ilivyo, mfano housegirls kutunza nyumba na familia wamesaidia baba na mama mwenye nyumba kwenda kazini [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4] , wafanya biashara ndogo ndogo wanasaidia mzunguko wa pesa mtaani n.k, wale wanaofanya kazi kwenye Ajira rasmi,wanategemea sana wale ambao hawako kwenye ajira rasmi/ informal sector,hivyo WOTE wapewe pensheni, sema wale waliofanya kazi na ku contribute wapewe extra for their services.

Mnaonaje?
Wazo zuri ila ubaya tu ni kwamba watasema co vipaumbele vyao katika utawala. Japo wawapatie huduma muhimu bure mfano.nadhani wazee wanabima za afya ..?
 
Back
Top Bottom