Na yule aliyetafsili maana yafisadi ni mtu anayechukua wake za watu
Kazi kweli kweli
Ni mimi hapa, tena huyo ni fisadi kweli kweli, kuliko hata anaefisadi mali.
Napenda ufahamu kuwa neno fisadi linatokana na lugha ya kiArabu na kwa waIslam ambao wengi wao huanza kufundishwa Qur'an tangu wakiwa watoto wadogo, maana ya neno fisadi haiwapi shida. Tatizo ni kwa wale waliolisikia neno fisadi ukubwani.
Neno Fisadi linamaanisha yule anefanya kitendo chochote cha uhalifu na uharibu kwa kuzidisha. Kwa mfano, kuna mtu anafanya ngono na mtu waliokubaliana na wote si mke wala mume wa mtu, hawa ni wafanya dhambi ya kujamiiana hawajafikia kuwa mafisadi. Lakini, mtu anaefanya uzinzi na mke au mume wa mtu, huyu ni fisadi.
Mtu anaeiba, si tu kwa njaa. Bali kwa kuwatia na hasara kubwa wengine, huyu ni fisadi pia.
Mtu anaewinda, si tu kwa yule mnyama akamla, bali akamuuwa ale nusu kilo na kilo 90 aziache ziharibike, huyu ni fisadi pia.
Anaetupa taka barabarani na pipa la taka lipo, huyu ni fisadi wa mazingira.
Anae wafanyia ufataki watoto wa wadogo na wa shule, huyu ni fisadi pia.
Natumai umeelewa.