Waziri atoa wito kwa jamii kuongeza juhudi katika kusoma vitabu ili kukuza maarifa

Waziri atoa wito kwa jamii kuongeza juhudi katika kusoma vitabu ili kukuza maarifa

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Uchukuzi, Atupele Mwakibete ameihamasisha jamii kuongeza juhudi katika kusoma vitabu ili kukuza maarifa yao.

Sambasamba na hilo Mwakibete amesema usomaji wa vitabu unaisaidia jamii kupata mbinu mbalimbali za uongozi katika ngazi zote.

JP5A1144.jpg

Mwakibete aliyasema hayo Desemba 16, 2022 katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Uongozi kiitwacho Leadership Through My Lenses).

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari na Teknolojia ya Mawasiliano, Nape Nnauye, Mwakibete alimpongeza mtunzi wa kitabu hicho Violet Mordechai.

“Uongozi unatafsirika kwa njia tofauti, siri kubwa ni kupata vitabu vyenye simulizi za kusisimua za uongozi na kuvisoma kisha kuyaishi yale uliyoyasoma yakuongoze kwenye shughuli zako.

JP5A1162.jpg

Mwakibete aliongeza kusema: "Nimekisoma ni kitabu kizuri naomba nakala za kitabu hiki zisambazwe kwenye ofisi na taasisi za umma ili nao wayaishi haya yaliyoandikwa humu.

“Hongera sana Violet kwa uandishi na ubunifu mkubwa ulioutumia katika kuandaa kitabu hiki,” alisema Naibu Waziri Mwakibete ambaye kwenye hafla huyo alimwakilisha Waziri wa Habari na Tehama, Nape Nnauye.

Naye mtunzi wa kitabu hicho Violeth aliwashukuru waliohudhuria katika hafla hiyo: uzinduzi huo huku akisisitiza ujumbe uliomo katika kitabu hicho kwamba uongozi ni kuonesha njia.

Katika uzinduzi huo muongoni mwa vitabu vilivyokabidhiwa kwa Naibu Waziri viliendelea kuuzwa ndani ya ukumbi huku akitoa ahadi ya kuvitumia vitabu hivyo wakati wowote pale itakapohitajika katika taasisi za serikali na umma kwa jumla.
 
Watu hawoni manufaa ya kusoma
Unajua unaweza ukawa unasoma vitabu for good motivation lakini unapata poor results
Maana waliosoma wenyewe wanadhihirisha kuwa kule ni majalalani
Motisha ya kusoma inakufa kabisa
 
Hakuna wasomaji vitabu siku hizi
We waambie mambo ya ubongo na fleva tu

Ova
 
Habari nzima haijasema Violet Mordechai ni nani, ana uzoefu gani, na kwa nini ni muhimu kusoma kitabu chake.

Nina vitabu kama 1,000 katika reading list yangu, kwa nini nisome hiki na kuacha vingine?
 
Back
Top Bottom