Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amefanya mabadiliko ya nafasi ya Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wa mkoa wa kihuduma Kibamba kutokana na kutoridhishwa na utendaji wake.
Mabadiliko hayo ameyafanya Novemba 28, 2025, baada ya kufanya ziara ya kikazi katika eneo la Mpiji Magohe, wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam ambapo aliwasilishiwa uwepo wa kero ya huduma ya maji na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa eneo hilo.
Waziri Aweso ameonesha kutoridhishwa na majibu ya Meneja wa DAWASA Kibamba, Mkashida Kavishe na kuamuru kuondolewa kwake na kuelekeza aletwe Meneja mwingine atakayesimamia majukumu hayo kwa ufanisi.