Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Waziri Aweso kwa Mamlaka aliopewa na Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na. 5/2019 amemteua CPA Sais Andongile Kyejo kuwa Mkurugenzi Mtendaji MORUWASA.
Ndugu Kyejo alikuwa ni Mkurugenzi wa Fedha Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) na atachukua nafasi ya Eng Tamimu Katakweba aliekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA.
Aidha, Waziri Aweso amemuelekeza katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuunda timu maalumu ya Wataalamu watakaofanyia kazi changamoto za hali ya huduma ya upatikanaji wa Maji Manispaa ya Morogoro na maeneo yote yanayohudumiwa na MORUWASA katika kipindi ambacho utekelezaji wa Mradi mkubwa wa Maji unaendelea.
CPA Sais Andongile Kyejo
~ Waziri Aweso unasema DAWASA kuna hujuma? Njoo Morogoro, huduma ya Maji ni kero kubwa
~ Morogoro: Meneja wa MORUWASA asimamishwa kazi