Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso leo Alhamisi tarehe 8 Mei 2025, atawasilisha Bajeti ya Mageuzi Sekta ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 Bungeni jijini Dodoma.
Mafanikio ya Sekta ya Maji yamechochewa na Uongozi wa Rais Samia na Wabunge – Miradi zaidi ya 2,300 imekamilika, upatikanaji wa Maji wapanda
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema mafanikio makubwa yanayoshuhudiwa katika sekta ya maji nchini yanatokana na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mchango wa wabunge, huku akibainisha ongezeko la bajeti kutoka Shilingi bilioni 680 mwaka 2021/22 limesaidia kukamilika kwa miradi mikubwa nchini.
Wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Mageuzi ya Sekta ya Maji kwa mwaka wa fedha 2025/26, Aweso amesema: "Waswahili husema, usione vyaelea, vimeundwa. Napenda kusema kwa dhati ya moyo wangu, waundaji wa mafanikio haya ni Mheshimiwa Rais na ninyi Waheshimiwa Wabunge."
Amesema miradi mikubwa ya muda mrefu sasa imekamilika ikiwemo Same–Mwanga–Korogwe, Mugango–Kiabakari–Butiama, pamoja na miradi 177 ya maji vijijini maarufu kama "miradi chechefu''.
Waziri Aweso ametaja pia miradi mikubwa ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa, ikiwemo mradi wa maji wa miji 28, Bwawa la Farkwa, mradi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi mkoani Simiyu, mradi wa maji kutoka Kahama hadi Ushetu, mradi wa Dambia–Haydom, mradi wa Ukirigulu–Koromije–Sumve, na mradi wa mazingira na maji katika jiji la Tanga na wilaya za Muheza, Pangani na Mkinga mkoani Tanga.
"Jumla ya miradi ya maji 2,331 imekamilika ambapo 1,965 ni ya vijijini na 366 ni ya mijini na hivyo kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kutoka wastani wa asilimia 70.1 mwaka 2020 hadi asilimia 83 mwezi Desemba, 2024 na maeneo ya mijini kutoka wastani wa asilimia 84 hadi asilimia 91.6."
"Kuanzishwa kwa RUWASA kumejenga miradi 3,379, na kupeleka huduma ya maji katika vijiji 10,517 kati ya vijiji zaidi ya 12,318. RUWASA imefanya mapinduzi makubwa katika kujenga na kuboresha huduma ya maji vijijini"
"Wizara imeendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo ya mijini ambapo miradi 68 yenye uwezo wa kuhudumia wananchi 3,362,850 imekamilika. Baadhi ya miradi iliyokamilika ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa mtandao wa usambazaji maji na matanki ya kuhifadhia maji Kusini mwa Dar es Salaam unaohudumia wananchi wapatao 450,000 wa maeneo ya Bangulo, Mwanagati, Kitunda, Kipunguni, Majohe, Kivule, Magole, Msongola, Chanika, Chalambe, Kinyerezi na Kifuru; Mradi wa Maji Mugango-Kiabakari-Butiama unaohudumia zaidi ya wananchi 100,000; na Mradi wa Maji Same-Mwanga- Korogwe uliozinduliwa rasmi na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 9 Machi, 2025 na unahudumia wananchi wapatao 456,900."
Bajeti ya Wizara kuongezeka kutoka Tsh. Bilioni 680 Mwaka 2021/22 hadi zaidi ya Tsh. Trilioni moja
Aweso: Vijiji 1,500 hazijafikiwa na huduma ya maji ni kati ya 12,318
Akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Maji kwa Mwaka 2025/2026, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Serikali imefikisha huduma ya maji.