Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, akijibu hoja ya Mdau kuhusu uhana wa Maji Kijiji cha Bukundi, amesema Taarifa hiyo sio ya kweli katika muktadha wa uhalisia ulivyo katika Mradi huu uliopo mkoani Simiyu.
Awali Mdau wa JamiiForums.com alidai kwamba, "Sisi wakazi wa Kijiji cha Bukundi Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, ambapo Serikali ilitekeleza Mradi wa Maji ambao tuliambiwa thamani yake ni Sh. Milioni 500 kisha ukafanya kazi kwa muda wa miezi mitatu tu, tunaomba kujua hatma ya mradi huu na huduma ya maji kwenye kijiji chetu."
Hapa chini ni Majibu ya Waziri kuhusiana na hoja hiyo.
" Ukweli wa mambo ni kwamba, Mradi wa maji wa Bukundi ni Kati ya miradi wa maji iliyopo Wilayani Meatu.
Mradi unahudumia wakazi 6344. Mradi wa maji ulijengwa na kukamilika kutoa huduma Mwaka 2016.
Mradi wa maji Bukundi unasimamiwa na Chombo cha watoa huduma ya Maji Nkoma ambapo jumla ya wateja 105, Taasisi 5 na Vituo 3 ambapo bill iliyotolewa Mwezi wa 8 hadi 11 Mwaka 2024 ni Tsh 4,028,000/= (MAJiS-CBWSO)
MABORESHO YA MRADI
Mradi ulikuwa na changamoto ya chanzo na bomba lililopita mtoni. Mwaka 2023 tulifanya maboresho katika maeneo hayo kwa kuchimba kisima chenye kina cha mita 20, kulaza mabomba yakuvuna maji mto Mwangadula ili kuongeza wingi wa maji kwenye kisima na kulaza bomba mtoni ambalo linapeleka maji kwenye tank.
CHANGAMOTO/UTATUZI
Kutokana na hali ya mvua kubwa zinazonyesha ,Mnamo tarehe 1-12-2024, bomba linalokatiza mtoni lilifukuliwa na kusombwa na mafuriko. Kwasasa tunasubiri mto upungue tuweze kurejesha huduma.
Hivyo huduma ya maji haipo katika kijiji cha Bukundi Kuanzia tarehe 1-12-2024 na siyo kwa muda wa kuanzia mwaka 2017 kama ilivyoripotiwa."
Jumaa Aweso
Waziri wa Maji