Waziri Aweso na Mkurugenzi Mkuu DAWASCO tusaidieni wakazi wa Mbezi

Waziri Aweso na Mkurugenzi Mkuu DAWASCO tusaidieni wakazi wa Mbezi

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
2,971
Reaction score
6,607
Waziri wa Maji pamoja na Mkurugenzi mkuu wa DAWASCO tunaomba mtukwamue sisi wakazi wa Mbezi hasa Mpiji, Msumi na Msakuzi ambao DAWASCO na wafanyabiashara wa magari ya maji wamekuwa wanatupa mateso sana.

Ni dhahiri kutokana na watendaji wa DAWASCO na wafanyabiashara inaonekana hawataki kabisa maeneo haya yapate maji.

Wapo wananchi wamelipia muda mrefu sana kuunganishiwa maji lakini imekuwa ni kupigwa kalenda kila siku, na wapo ambao wameunganishiwa mabomba lakini wanapata maji mara moja kwa miezi hata mitatu.

Bahati mbaya sana baadhi ya wenye magari ya kuuza maji ni watu tunaowafahamu na wanakuwa wazi kuwa kuna percent wanawapatia mabosi wa DAWASCO hasa injinia wa maji.

Na huenda hawa watendaji wa DAWASCO wanafanya hujuma hizi pasipo viongozi wakuu wa DAWASCO kujua
 
Kweli huko kwa ribaba maji shida sana...

Ova
 
Huko mpiji malalamiko ni mengi sana
Maji
Barabara mbovu
Usafiri wa tabu sana

Yan huko sijui ni lini patapewa kipaumbele
 
Back
Top Bottom