Songambele
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 4,710
- 2,587
Hapa ndio nawakubali wamatumbi nyie ni kufahamu zaidi kwanini nyinyi ni maskini, ushashiba maharage hapa unabandle lako la kuunga uunga ukaamua nawe utoe mchango wako wa kujenga taifa hili lenye watu wengi msiojitambua. Mie mwenzio nilidhani ungeona haja ya watu kukusanya nguvu wizara zote na kukamilisha huu mradi kwanza utaongeza uzalishaji, pili vijana watapata fursa ya kutumia vipaji na nguvu zao na mwishi watatengeneza ajira zao na wenzao.Waziri Bashe tumeona kwa miezi kadhaa umezindua program inaitwa BBT (Building Better Tomorrow), ambayo itafanywa na wizara ya Kilimo kwa ajili ya vijana , hii ni Kuingilia majukumu ya Wizara ya VIJANA, AJIRA ,KAZI na WATU WENYE ULEMAVU.
Hii unayofanya kwenye BBT ni Skills development na Capital creation ambayo sio kazi ya Wizara ya Kilimo ni kazi ya Wizara ya VIJANA, maana wizara ya vijana ndio imekuwa na jukumu la kuandaa program mbalimbali kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana na kuwakopesha mitaji, hii wamekuwa walifanya kwa ushirikiano na wizara ya TAMISEMI, KILIMO n.k
Bashe tunakuomba jikite na kukikwamua kilimo ambacho kinakufa mikononi mwako maana stakeholders wengi wa kilimo unawavuruga na hii kupelekea wengi kukaa kimya wakikuangalia tu
Tangu lini wizara ya Kilimo ikahusika na Skills development ya vijana kama unavyofanya kwenye BBT?
Nakushauri jikite kwenye kuwezesha wakulima Wapate mikopo kwa hati za kimila au kubwa ba sio kwa dhamana ya nyumba, jikite kuwavutia watu wapende kilimo na sio kuwakatisha tamaa.
Pia nyakati zinabadilika sana. Kuna kampuni za kilimo zinahusika na kuwalimia watu, hawa ni wadau wa kilimo Kaa nao uwasikilize na kujua changamoto zao na Serikali Ione inawasaidiaje na sio kuwatukana kila siku huku serikali hiyohiyo imewasajili hadi soko la DSE, na hizi kampuni nyingine zimezinduliwa hadi na viongozi wakubwa wa Serikali akiwemo Waziri Mkuu mmoja mstaafu, hivyo kama kuna makosa ukae nao na kurekebisha na sio kutoa vitisho maana unaua sekta ya Kilimo wewe Mwenyewe
Jikite kwenye kutatua changamoto sio kutuhumu, Hadi sasa Kuna changamoto za MBOLEA, upungufu wa chakula leo hii kilo ya unga ni 2000, mchele ni 3500, maharage ni 4500. Je, ni Watanzania wangapi Wana mudu hizi gharama?
Ukiona watu wameingia kwenye Kilimo Waite wasaidie wanapokwama ili uzalishaji uwe mkubwa zaidi.
Program ya BBT wizara Yako ikabidhini wizara ya Vijana, Ajira na Kazi ndio inatakiwa iwe huko nyie wizara toeni msaada wa kitaalam na sio kuiendesha sio kazi ya Wizara ya Kilimo.
Sie wahafidhini tuliona taabu na siasa ya kupata hao vijana manake huku mtaani tunaona wajumbe wa CCM wanataka kutupeleka kule kule kwa zile pesa za 10% na miradi mingine iliyowekwa siasa ikafeli. Wazo lako sio baya ila likague tena uone kama bado lina tija au lifute tufanye mambo.