Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amempongeza Mbunge wa jimbo la Ushetu Mhe Emmanuel Cherehani kwa kuendelea kuonyesha uzalendo katika kuendeleza sekta ya Kilimo.
Waziri Bashe ameeleza hayo wakati akizungumza na Wananchi wa kata ya Ushetu akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Shinyanga ambapo amesema Mbunge Cherehani ni mpambanaji katika maendeleo ikiwemo sekta ya Kilimo hivyo ni mfano wa kuigwa.
“Mwaka 2019 nilipoteuliwa na Hayati Magufuli na Mama Samia kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, nilijua Cherehani atachukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo hili, na yeye anajua nilimwambia ukija bungeni ukawa unakaa tu huangaikii matatizo ya Wananchi wako daima usiwe rafiki yangu na daima sitokuunga mkono, lakini leo hii ameonyesha uzalendo na upiganaji kweli kweli hasa kwa wakulima wa Nchi hii”,amesema Bashe
Ameeleza kwa utani kuwa “Cherehani hayupo peke yake, sio mwepesi kama mnavyoliona umbo lake, sisi tupo nyuma Yake, tunaamini anasimamia maslahi ya Wakulima wote wa Jimbo hili na tutamuunga mkono”.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe Emmanuel Cherehani ameiomba Serikali kupitia Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe kuona umuhimu wa kutenga eneo kwa ajili ya kufugia ili wananchi waweze kuzalisha mifugo ya kisasa na kuendelea kuchangia pato la Taifa.
‘’Mkoa wa Shinyanga tunawafugaji wengi na tuna mapori ya kwetu lakini wafugaji wetu hawajawahi kutengewa hata robo heka kwa ajili ya machungio, na mgogoro kati ya wafugaji na wakulima ni mkubwa, tunaomba serikali yetu tutengewe eneo la kuchungia ili tuzalishe mifugo ya kisasa tuweze kuchangia pato la Halmashauri na Taifa kwa ujumla” Amisistiza Mbunge Cherehani
Hata hivyo ameiomba Serikali kupunguza gharama ya Mzigo wa miti ya tumbaku ili kuweza kuzalisha zao hilo kwa wingi.
Mhe. Cherehani ameiomba Serikali kutengewa eneo la mradi kwa ajili ya umwagiliaji ili Wananchi wazalishe mazao, na ajira zipatikane kupitia mradi huo.