Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ametoa Kauli ya Serikali sakata la Kupiga Marufuku kuuza Mazao ya Nje.
Waziri Bashe amesema Mazao ya Kilimo ni kama biashara zingine hivyo Serikali imeamua kurasimisha biashara ya mazao ya Kilimo kwa kuwataka exporters na Wageni wote kusajili kampuni Kwa Kasi hiyo ndio waruhusiwe kwenda kununua mazao kwa wakulima maana Serikali inahitaji Mapato na kuona sekta ya Kilimo inachangia kwenye mapato ya Nchi.
My Take: Hapa Sasa mumeeleweka na naunga mkono hoja Kwa ubunifu huu.
====
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kilichozuiliwa na Serikali ni watu kufanya biashara ya mazao kinyume na utaratibu.
Bashe amesema havo alipokuwa akizindua Ofisi va kuleta mabadiliko ya sekta ya kilimo nchini jijini Dodoma leo jumatatu Juni 19, 2023 ambapo ameeleza kuwa Serikali haitaruhusu mtu yeyeyote kusafirisha mazao nnje ya nchi ikiwa hajasajili kampuni, hana Tin namba, Taarifa za ulipaji kodi pamoja na leseni ya biashara husika.
Chanzo: Mwananchi