Waziri Bashe, TADB wanakopesha wakulima gani?

Waziri Bashe, TADB wanakopesha wakulima gani?

Unitman

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
511
Reaction score
671
Habari ndugu wanajamii.Kuna benki inajiita ya kilimo tanzania hawa jamaa sijuhi wanakopesha wakulima wa nchiiii gani??Au ipo kisiasa na kimtego kuadaa wananchii.

Ukienda pale watakwambia uende kwenye benki za biashara kwamba wanamakubaliano nao kukopesha wakulima na Wafugaji.Lakini kule benki hakuna maelekezo yoyote wanataka uwe na biashara na ulejeshe kila mwezi ishu za kilimo na Mifugo hazijulikani popote labda wakulima wakubwa tu ndo inawezekana wanapata Lakini Sisi wadogo hatuna chetu sasa tutakuaje bila kuwezeshwa kama mnathamini wazalishaji wakubwa?

Naamini kama serikali imeweka fedha kukopesha wakulima watakuwa wanakopeshana wenyewe kwa kujuana sasa wanamkomoa Nani ikiwa tunaendelea kuwa masikini na kukosa ajira?

Utawala wao utakuja kupata mshutuko iwapo wataendelea kuzalisha umasikini na kufaidisha wachache?

Waandishi wa habari na nyie siku hizi mnapenda habari nyepesi na za udaku ingieni mtaani mfanye utafiti kujua TADB wamekopesha wakulima WANGAPI?

Au Halimashauri wamekopesha vijana,walemavu au wamama WANGAPI?

Ukiwaomba taarifa watakupa hewa hivyo tafuteni ukweli wanakopeshana wenyewe kwa wenyewe HAKUNA kitu HAPO ...
 
Mi ni mfugaji wa ng'ombe wa kisasa ila sijui napataje mkopo?
 
Hii mikopo inaishia kwa watu ambao hata siyo wakulima na hata shamba,mbolea hawalijui,ila ndiyo wanaokula hela tu

Ova
 
Back
Top Bottom