baba anjela
JF-Expert Member
- Mar 17, 2013
- 431
- 310
Mh Bashe , wewe ni miongoni mwa mawaziri mnaochapakazi na zinaonekana, hongera sana.
Ombi langu kwako nalielekeza kwenye maduka ya pembejeo za kilimo na mifugo...kwakweli kumejaa makanjanja wengi sana. Wauzaji wao wengi hawana utaalamu wa kilimo au mifugo.
Na wale walio na wataalamu basi ni level ya diploma au certificate... na kichwani mwao sifuri tupu. Wewe jaribu kufanya utafiti wako binafsi utagundua jinsi wakulima na wafugaji wanavyopata hasara kubwa hasa katika upande wa madawa mpaka upate dawa sahihi ya ugonjwa utajikuta umenunua dawa tofauti zaidi ya tatu au nne ni kama vile wanabahatisha katika kutibu ugonjwa...na hapo unakuta dawa moja si chini ya 13, 000 sasa piga hesabu , mpaka unavuna au unapeleka kuku sokoni umeingia hasara kiasi gani, wao ni chanzo cha mifugo kufa au mazao kuharibika.
Nilijaribu kufanya utafiti mdogo tu...ni lilima matikiti maji , ukaingia ugonjwa (mdudu mafuta) nikachuma matawi kama matano nikapeleka hiyo sample maduka kama kumi tofauti cha kushangaza maduka yote yalinipa majibu tofauti tofauti na dawa tofauti hakuna majibu yaliyofanana kabisa.
Mh Bashe, jaribu kutazama kwa jicho la tatu. Haya maduka yanachangia sana vijana wengi kuona kilimo na ufugaji ni hasara na hakuna faida.
Haya maduka wanatengeneza faida sana , nijukumu la serikali kuwawekea utaratibu juu ya wataalamu wao na ikibidi kuwafanyia snap check mara kwa mara ili kulinda uduma bora.