The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeagizwa kushirikiana kwa karibu na Idara ya Uhamiaji na Idara ya Wakimbizi ili kubaini waomba vitambulisho vya taifa wanaoikidhi vigezo vya kupatiwa vitambulisho hivyo hususani kwa kwa wananchi wa mikoa ya pembezoni na kuwapatia kwa haraka.
Maagizo hayo yametolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa kwenye mkutano wa kutathmini utendaji kazi ya mamlaka hiyo sambamba na kupanga mikakati ya uboreshaji wa huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo.
Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
“Shirikianeni na Idara ya Wakimbizi na Uhamiaj katika kushughulikia kwa haraka na ufaninisi bila kuvunja sheria maombi ya wananchi wa mikoa kama Kigoma na Kagera na wasiokidhi vigezo wataarifiwe kwa wakati na wenye vigezo wapewe kwa haraka” amesisitiza Bashungwa.
Mbali na msisitizo huo pia Bashungwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa NIDA kuongeza ubunifu ili wamiliki wa vitambulisho vilivyochapishwa wakabidhiwe mapema.
Kwa mujibu wa NIDA kufikia tarehe 10 Februari 2025 vitambulisho 1,507,796 vimesomeshwa kwenye mfumo na wamiliki wa vitambulisho 918,216 wameshatumiwa ujumbe mfupi ili kuchukua vitambulisho vyao.
Chanzo: Azam TV