Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Bashungwa ameelekeza hayo leo tarehe 23 Januari 2025 wakati alipofanya ziara Makao Makuu ya dara ya Uhamiaji, Dodoma ambapo ameitaka Idara hiyo kuendelea kuboresha utoaji huduma kwa Wananchi.
Soma: NIDA kusitisha matumizi ya namba kwa wasiofuata vitambulisho vyao
Bashungwa amemtaka Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji CGI, Dkt. Anna Makakala kuhakikisha kila Ofisi ya Wilaya ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa inakuwa na Afisa wa Uhamiaji ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Aidha, Bashungwa ameiagiza Idara ya Uhamiaji kuendelea na Operesheni, misako na doria za kukamata wahamiaji haramu na kuhakikisha wageni wote wanaoingia ndani ya nchi, wanafuata tararibu na sheria za kuingia nchini.
Kadhalika, Bashungwa ametoa onyo kwa baadhi ya Maafisa wa Idara ya Uhamiaji ambao sio waaminifu, wanaowaonea Wananchi wakati wa Operesheni na misako inapofanyika
Awali, Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji CGI, Dkt. Anna Makakala ameeleza kuwa Idara ya Uhamiaji inaendelea na misako, doria na kaguzi mbalimbali kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa.
Nimeelekeza Idara ya Uhamiaji na NIDA kushirikiana ngazi za wilaya maafisa wote wa NIDA na Uhamiaji wawepo ofisi moja wakati wanahudumia wananchi ili kuondoa usumbufu wa wananchi kutoka ofisi moja kwenda nyingine na wakati taasisi zote 2 zipo ndani ya Wizara moja na wilaya moja. Nitakapokuwa napita huko kwenye wilaya tutasimamia ipasavyo utekelezaji wa hili jambo kupitia mrejesho wa wananchi.
Soma:
~ Daniel Sillo: Uhamiaji ongezeni kasi ili watu wapate Vitambulisho vya NIDA
~ Huduma mbovu watumishi kupitia Uhamiaji na NIDA chanzo cha ucheleweshaji wa huduma Kitambulisho cha Taifa