Waziri Bashungwa atembelea Shirika la Mzinga, apongeza kuongezeka uzalishaji mazao

Waziri Bashungwa atembelea Shirika la Mzinga, apongeza kuongezeka uzalishaji mazao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2022-12-13 at 10.00.07 PM.jpeg
Waziri wa Ulinzi na JKT, Innocent Lugha Bashungwa (Mb) amesema anajivunia kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la msingi katika Shirika la Mzinga.

Ameyasema hayo Disemba 13, 2022, alipofanya ziara ya kutembelea Shirika hilo.

Hiyo ni ziara ya kwanza kufanywa na Waziri Bashungwa katika Shirika la Mzinga kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Shirika hilo ambalo ni moja ya mashirika chini ya Wizara yake, tangu ateuliwe na kuapishwa rasmi na Samia Suluhu Hassan, kuwa Waziri wa Ulinzi na JKT tarehe 03 Oktoba, 2022.

WhatsApp Image 2022-12-13 at 10.00.06 PM.jpeg
Akiwa katika Shirika hilo alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali na kujionea shughuli zinazoendelea, ambapo aliweza kupatiwa maelezo ya kina kuhusu maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na hatua zilizofikiwa katika kuzalisha mazao ya msingi, kuangalia matokeo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka mitano (2017/18 - 2021/22), mafanikio yaliyopatikana, changamoto na mipango waliyojiwekea.

Maeneo aliyoyatembelea ni pamoja na Kiwanda kinachozalisha mazao mbalimbali, ya msingi na mbadala, karakana, kuangalia maboresho ya hospitali ya Shirika yenye hadhi ya Wilaya pamoja na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Baadhi ya mafanikio ya Shirika ni pamoja na utengenezaji wa risasi za kuwindia wanyama, kuendelea kuagiza na kuuza silaha zenye kaliba ndogo, kuendelea kutekeleza miradi ya ujenzi kupitia Kampuni Tanzu ya Mzinga Holding Company Limited, kukamilika kwa nyumba ya kulala wageni Magadu Hotel pamoja na maboresho ya Hospitali ya Shirika na Mzinga Vocational Training Centre (MVTC).

WhatsApp Image 2022-12-13 at 10.00.08 PM.jpeg

WhatsApp Image 2022-12-13 at 10.00.10 PM (1).jpeg
Akitoa taarifa ya Shirika kwa Waziri, Meneja Mkuu, Brigedia Seif Hamis alisema Kuwa Shirika la Mzinga lilianzishwa rasmi mwaka 1971, ukiwa ni mradi kwa ajili ya kuzalisha mazao kwa matumizi ya JWTZ. Na ilipofiika tarehe 13 Septemba, 1974 mradi huu ulibadilishwa na kuwa Shirika la Umma (Public Corporation) chini ya Wizara ya Ulinzi na JKT kwa Tamko la Serikali Na. 219.

Aidha, Brigedia Jenerali Hamis aliongeza kusema kuwa Shirika la Mzinga kisheria linao wajibu wa kuzalisha mazao ya msingi na mitambo, kufanya tafiti mbalimbali, kukarabati vifaa na mitambo mbalimbali na kutekeleza majukumu yote muhimu kwa maendeleo ya Shirika na Taifa kwa ujumla.

Shirika la Mzinga linajishughulisha na shughuli kuu mbili, kwanza, ni shughuli za kuzalisha mazao ya msingi ya mwaka 1971 na yale mazao yaliyoongezwa mwaka 2012 ambapo uzalishaji wake umeongezeka kutoka asilimia 11 hadi kufikia asilimia 87 mwaka 2022. Pili, Shirika pia, linajishughulisha na shughuli za uzalishaji mazao mbadala ili kujiongezea kipato kwa lengo la kupunguza utegemezi wa ruzuku kutoka Serikalini.

Shirika la Mzinga lilianzishwa mnamo mwaka 1971 kama mradi wa mazao ya msingi chini ya Makao Makuu ya Jeshi kwa ajili ya kuzalisha mazao kwa matumizi ya JWTZ. Ilipofika tarehe13 Septemba, 1974 mradi huu ulifanywa kuwa Shirika la Umma (Public Corporation) kwa Tamko la Serikali Na. 219.

WhatsApp Image 2022-12-13 at 10.00.09 PM (1).jpeg

 
Kwani Tanzania tunazalisha makombora ya aina gani ambayo yanaitwa mazao msingi?
 
Kukagua mazao kwenye shirika la mizinga?
Au "mizinga" inaana zaidi ya moja.
 
Ili majeshi yetu yalingane na majeshi makubwa inabidi serikali iruhusu sekta binafsi kuwekeza kwenye utengenezaji wa zana za kivita kisha kuwauzia jeshi.
Jeshi haliwezi fanya kila kitu.
 
Eti!!?

Anafiti KABISA na lile chapisho la jamaa yetu kwamba "patriotic, calm, intelligent, visionary, truthfully and humble"!!?

Lakini kuna Jamaa anasema tofauti japo matokeo ya UNEC yanamfavor KABISA!

Japo ukiangalia matokeo yale kuanzia namba 1 hadi 10 ,yule wa KUMI akiambiwa nyumaaaa!!Geukaaàaaa!!! Anakuwa wa KWANZA!!
 
Hii habari haina maana yoyote kuileta hapa maana habari nzima imejaa neno 'mazao' ya msingi bila kutaja ni mazao gani.

Na kama hayo 'mazao ya msingi' ndio hayo m waliyoshika hapo kwenye gwaride basi bado sana.
 
Mdaraka shkamoo, jamaa kanona wacha kabisaa 🤣 🤣
 
Hii habari haina maana yoyote kuileta hapa maana habari nzima imejaa neno 'mazao' ya msingi bila kutaja ni mazao gani.

Na kama hayo 'mazao ya msingi' ndio hayo m waliyoshika hapo kwenye gwaride basi bado sana.
Mkuu

Hizo ziara ni za kumfanyia screening au interview mlengwa KWA kazi Fulani KUBWA!

Amekua akihamishwa wizara Sana tena KWA muda mfupi!

Alimtoa waziri wa kike kitini je atamtoa nani wa kike tena kitini Ili yeye akae!

Ngoja Tuone,wizara Hii ni nyeti Sana!
Sio bure,Huwa hawawekwi wanasiasa Hapo wanawekwa watu calm na secrecy!

Ngoja Tuone
 
Mkuu

Hizo ziara ni za kumfanyia screening au interview mlengwa KWA kazi Fulani KUBWA!

Amekua akihamishwa wizara Sana tena KWA muda mfupi!

Alimtoa waziri wa kike kitini je atamtoa nani wa kike tena kitini Ili yeye akae!

Ngoja Tuone,wizara Hii ni nyeti Sana!
Sio bure,Huwa hawawekwi wanasiasa Hapo wanawekwa watu calm na secrecy!

Ngoja Tuone
Ok sawa
 
Jeshi la JWTZ kikosi cha kilimo sio kikosi cha mizinga.

Tuna kila sababu ya kulifanyia reform kubwa sana jeshi hili la JWTZ liwe la kisasa sio kama lilivyo sasa.
 
Back
Top Bottom