Waziri Bashungwa awataka wamiliki wa redio kulipia muziki wanaopiga

Kwahiyo Eminem na Outkast watawatumia pesa zao hukohuko USA?
 
Usiku wapige nyimbo laini mpaka panya nao walale
 
Tayari zinalipwa tangu enzi za magu..tena enz za magu ilikua laki nne kwa mwaka ila mwaka huu naona imekuja laki mbili na ndan ya siku 35 uwe ushalipa!

Chakusikitisha ni kuwa wamiliki wa redio wanatumia sana mitandao ya simu..wateja wao hasa redio jamii unawza kuta kwa siku mtu kajiunga kifurushi na kinaishia kupiga simu redioni au kutuma meseji na wamiliki wa redio washatuma maombi mengi sana tcra wasimamie hili jambo ili wamiliki nao angalau wapate asilimia kadhaa toka kwenye mitandao lakin tcra cjui hata wanafanya nini? Utasikia nenda mwenyewe kwenye makampuno ya simu ukaombe khaaaa
 
Hao wasanii idadi yao ni ngapi? je kama nyimbo yangu haikupgwa kbs ktk mwwz huo je nitalipwa?kma msanii nymbo zake zimepgwa mara chache tu je atalipwa sawa na yule wa zilzopigwa nying?
Hili jambo wanasimamia cosota..nadhani ni pesa inagawanywa sawa kwa wasanii inaeza isiwe kupewa pesa mkononi lakini ukaambiwa wasanii wanajengewa studio au cjui wanaboreshewa maslah..na ndiyo vivutio pia vya wasanii kujiandikisha ili na wao walipe kodi vizuri heehee
 
Haina shida wao waendelee kuota hizo ndoto zao na kukurupuka kutunga hizo sheria, mimi binafsi kwenye radio nayofanya kazi ntapiga ngoma za nje tu na ninazo nyingi haswaaa... Si wanataka kuua soko la muziki wa bongo na kubore wasikilizaji.

Serikali inashindwa kutambua ya kua hizi radio zinatumika kumpromote msanii na kazi zake tu, siku hizi kuna digital platforms nyingi huko mtandaoni ndiko hawa vijana wanapatia mpunga wa kutosha, kuna apple music hii wasanii ndo wanapiga hela sana, kuna boomplay, tidal, spotify n.k
 
hii kitu imewatafuna kenya,hawana hamu.
Kenya walijuta kuweka hii kitu, redio zao zilianza kupiga amapiano, reggae, nigerian music, na american hits tu... local music ulikua haupigwi sana ndo akili ikawakaa sawa kumbe walikurupuka...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…