Waziri Bashungwa: Wanaolalamika kuibiwa Simu wanakutana na Nenda rudi nyingi kituo cha Polisi

Waziri Bashungwa: Wanaolalamika kuibiwa Simu wanakutana na Nenda rudi nyingi kituo cha Polisi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema wananchi wamekuwa wakilalamikia ucheleweshaji wa upelelezi wa simu zilizoibiwa, hali inayowafanya wahalifu kuepuka kukamatwa kwa wakati ambapo ameagiza Jeshi la Polisi kushughulikia changamoto hiyo kwa haraka.

Bashungwa amesema Serikali itawezesha Kamisheni ya Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai kwa vifaa na mifumo ya kisasa ili kusaidia Jeshi la Polisi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Awali, Kamishna wa Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai, CP Shabani Hiki, amesema Kamisheni hiyo inaendelea kuboresha mifumo yake, Katika mwaka 2024, imefanikiwa kuchunguza vielelezo 21,905 vya kesi 1,858 pamoja na miili 411, na kubaini vyanzo vya vifo.

Pia soma ~ Dar es Salaam: Mchakato wa ufuatiliaji simu zilizoibiwa kupitia Vituo vya Polisi una ‘harufu ya michezo michafu’
 
Lazima uache laki ndipo upelelezi uanze mbaya zaidi kuna afande wa kike aliniambia ukweli ,kaka simu yako bei gani ,si bora ununue nyingine kuliko kupoteza muda wako kuja hapa Tanpol.
 
Lazima uache laki ndipo upelelezi uanze mbaya zaidi kuna afande wa kike aliniambia ukweli ,kaka simu yako bei gani ,si bora ununue nyingine kuliko kupoteza muda wako kuja hapa Tanpol.
Kabisa. Hata me ilinitoka laki 1 na simu siku ya pili tu nikaipata...wakati nilishasumbuka zaidi ya week 3 ati wanasema simu haijawashwa bado. Na wakati simu ilionesha imewashwa baada ya siku 5 tu kuibiwa.
Sema nashkuru laki yangu ilirudi maana na mie nilimkamua muibaji
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema wananchi wamekuwa wakilalamikia ucheleweshaji wa upelelezi wa simu zilizoibiwa, hali inayowafanya wahalifu kuepuka kukamatwa kwa wakati ambapo ameagiza Jeshi la Polisi kushughulikia changamoto hiyo kwa haraka.

Bashungwa amesema Serikali itawezesha Kamisheni ya Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai kwa vifaa na mifumo ya kisasa ili kusaidia Jeshi la Polisi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Awali, Kamishna wa Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai, CP Shabani Hiki, amesema Kamisheni hiyo inaendelea kuboresha mifumo yake, Katika mwaka 2024, imefanikiwa kuchunguza vielelezo 21,905 vya kesi 1,858 pamoja na miili 411, na kubaini vyanzo vya vifo.

Pia soma ~ Dar es Salaam: Mchakato wa ufuatiliaji simu zilizoibiwa kupitia Vituo vya Polisi una ‘harufu ya michezo michafu’
Majibu yao kuna mda bora ukanunue tu simu mpya 🙌
 
Simu wanakuwa wameishaipata ila hawasemi. Wataanza kuchukua hela kwako, halafu watachukua ndefu kwa waliyemkuta na simu na wala hawakupi taarifa kuwa wameipata. Watarudi kwako kukutaka uongeze hela, ukiongeza ndio wanakwambia tumeipata
 
Wizi wa simu umekithiri duniani na hata majuu imekuwa kero sana
Yaani unatembea na simu kijana anakuja na baiskeli ya umeme na kukupokonya, huyo anaondoka

Kufuatilia simu ni mda na gharama lakini wanaweza.
 
Jeshi la polis lijitathimini sana kwenye simu za wizi. Hapa moro kuna jamaa yangu ameibiwa simu na kuporwa pochi usiku wakati anatoka kulitumikia Taifa. Akaripot polis na polis wakaaza kumzungusha. Kuna afande akamtonya Akapanda kwa RCO akabadilishiwa mpelelezi. Kumbe yule mpelelez wa kwanza simu kaipata na kuiuza kwenye duka la jamaa yake Masika na kuuziwa mwanafunz wa SUA. Kwaiyo huyu mpelelezi mpya wakai track simu wakampata huyo mwanafnz wa SUA baada ya kubanwa akasema kainunua masika na walipoenda dukan mwenye duka nae akamtaja afande aliyemuuzia. Kilichofuata akapewa simu na hela yake na kuombwa yaishe ili yule afande asifukuzwe kazi.
 
Back
Top Bottom