Vyeo viwili kwa wakati mmoja kwa Biteko ndio changamoto. Ana mambo ya kiserikali na mambo ya wizara.
Mara nyingi anatumwa kwenda kufanya hiyo kazi na waziri Mkuu ama rais mwenyewe.
Matatizo ya wizara ya nishati yanajulikana na suluhisho lake linajulikana, Biteko hata awepo ofisini hakuna atakachobadilisha.
Kwa sasa wizara, TANESCO na nchi kwa ujumla matumaini yao ni Bwawa la Mwalimu Nyerere kuwashwa mwaka kesho ili umeme uwake, hakuna mbadala mwingine wowote ulioko hapa karibu wa kutatua changamoto ya umeme, hakuna.
Walioharibu ni kina Makamba na maharage, wamekaa pale miaka 2 mizima hakuna cha maana walichokifanya, wakashindwa hata kuanzisha mradi mmoja wa umeme wa solar ama upepo ambao ungeweza kukamilika ndani ya miezi 18 hadi 24. Wao wakakalia wizi, media coverage na publicity tu.