Waziri Biteko: Tuna vijana waliomaliza kidato cha sita ama digrii ya elimu fulani, lakini hawezi kujipikia chakula chake

Waziri Biteko: Tuna vijana waliomaliza kidato cha sita ama digrii ya elimu fulani, lakini hawezi kujipikia chakula chake

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema ni kawaida kuona mtoto amemaliza kidato cha sita ama digrii ya elimu fulani, lakini hawezi kajipikia chakula chake mwenyewe.

Amesema Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi sStadi (Veta) ina uwezo na jukumu la kubadilisha Tanzania kama jamii itakubaliana watoto kupataa stadi fulani kwa ajili ya kuboresha maisha.

Dk Biteko ameyasema hayo leo ljumaa Machi 21, 2025 wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Miaka 50 ya Veta iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 
Tulikuwa BTP katika shule moja tumechanganyikana wanaume na wanawake. ikifika zamu ya wanaume kupika ilikuwa chakula hakiivi tunaishia kumwaga. Kikundi kilikuwa na wanaume wasiojua kupika. Tukapangwa kazi tukawa na jamaa asiyejua kupika ikifika zamu yake anapika mataptapu tu iwe ugali, mboga au wali. Jamaa hakuwa na ustadi wa kupika chakula. Tuliopitia sayansi kimu tunajua kupika misosi
 
Tumechoka na hizi bwata bwata za viongozi kuhusu VETA, Wawapeleke kwani watoto wao, afu na sie wengine tutafata.

Mxxxxiiiieeew
 
Afu huyu n mbunge wangu kabisa, aje anilipie hzo gharama za veta niende geita mjini nikasome, anasema tu huku na mm nikajifunze kupika veta
 
Back
Top Bottom