Waziri Cha Pombe

Waziri Cha Pombe

Cynic

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2009
Posts
5,144
Reaction score
1,651
Jamani hebu angalieni maajabu!

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=lWLeWqPOFpU]YouTube - Japanese finance minister drunk at G-7[/ame]

Huyu ni Mkulo wa Japan (Japanese Finance Minister) alipokuwa kwenye News Conference wakati wa mkutano wa G-7 Rome. Halafu anakanusha hakuwa amelewa!

Bahati yake hakuna ''The Home of Great thinkers" huko...
 
mheshimiwa kazidiwa;aibu, aibu tupu. Wajapan wamebadilika sana siku hizi.
 
Kilaji wakati wa Press Conference?

Yaani alitaka kutoa nishai akazidisha nini?

Kwani hajuamini?
 
Ni aibu kweli, hasahasa wakati huo walipokuwa wanashughulikia economic meltdown. Lakini wenzetu maslahi ya taifa mbele - hatimaye kakubali kujiuzulu baada ya kupima na kuona uzito. Siyo TZ watu wana komaa kommaa hadi mambo yanasahaulika au kulialia na kusamehewa
 
Lakini sasa si alikuwa anaweza kujibu kwa ufasaha na kama ni hivyo hoja zake zinaweza zikawa ni kweli kwamba hakulewa. Wangapi sisi tunawaona wabunge wetu Dodoma wamelala na ukiuliza wanasema wanatafakari. Mfano Nakumbuka Mh Aliyekuwa Waziri wa Elimu ya Juu na wengine wengi kipindi cha Mkapa na sasa.

Ndio zao kama sio Bwaksi (Pombe) basi ujue Night Nurse (Dada Poa)
 
Amekana kuwa alikuwa matingas, ila ameamua kujiuzulu nafasi hiyo kuwaacha wengine wenye imani ya wananchi wafanye Gonga
 
tehe tehe waziri ni yuko tungi bovu......
 
.... alikana lakini, alisema alikunywa dawa..., lakini wenzetu kwa kuwajibika ni mara moja kaachia ngazi... sisi mmh mpaka pachimbike🙄
 
Mimi nadhani viongozi wetu wa Tanzania kama MAWAZIRI, WABUNGE, MAJAJI na Senior Executive woote katika ofisi ama taasisi za umma na wengine woote wenye dhamani kwa jamii wangeiga tabia ya waziri wa fedha wa Japan. Ukilewa ukiwa kazini, ukifumaniwa, ukifanya ufisadi n.k ni wewe mwenyewe unapima adhari za makosa na matendo yako kwa jamii na halafu unajiuzulu mwenyewe.
 
Back
Top Bottom