Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamurilo: Poleni sana kwa kumpoteza Injinia Patrick Aron Mfugale, mheshimiwa Rais tumesikia maelezo mengi yametolewa kuhusu elimu na ajira ya marehemu, tumesikia vilivile kuhusu mchango wake wa kitaalamu, tumesikia vilevile kuhusu tuzo mbalimbali ambazo amezipata kutokana na utumishi wake uliotukuka.
Vilevile tumepata ushuhuda kutoka kwa watoto na viongozi mbalimbali walioshiriki katika miradi ambayo ameisimamia, itoshe hapo nisiongeze mengine bali niseme nasi tuendelee kumuenzi katika yale aliyokuwa akiyafanya na tujitahidi kadri tuwezavyo kuhaulisha yale yote aliyoyasimamia ili nasi tuendelee kuyafanya kama alivyokuwa akiyatekeleza.
Mheshimiwa Rais, katika salamu za familia wameonyesha ombwe kwamba familia ilikuwa haifahamu ni jinsi gani limetokea na mimi kama msimamizi mkuu wa wizara ninawajibika kutoa maelezo mafupi.
Katika uongozi wa wizara tuna mikutano mbalimbali na ambapo tulikuwa na mkutano kati ya wizara na Tanroads siku ya Ijumaa wiki iliyopita ambao haukufanyika kwasababu marehemu aliomba kikao kisogezwe hadi Jumanne kwani alikuwa ana majukumu mengine ambayo kasababu hakuweza kuyaahirisha.
Kwasababu tunafanya kazi pamoja tuliridhia ombi hilo na kikao kilifanyika Jumanne kama ilivyopangwa, Jumanne tuliamka mimi nikaelekea Bungeni na katibu mkuu wangu sekta ya ujenzi aliongoza kikao hicho.
Katika kikao hicho majira ya saa nne, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya na ndipo katika mkuu akamueleza aende akapumzike katika ofisi jirani ambayo ni ofisi yake ili kikao kiendelee.
Aliamka mwenyewe bila usaidizi wowote na kwenda katika ofisi ya katibu mkuu sekta ya Ujenzi na kikao kiliendelea lakini katibu mkuu aliwaambia kwenye kikao endeleeni na kikao kwanza niende nikamuangalie mhandisi mfugale kisha tuje naye tuendelee na kikao chetu.
Katibu mkuu alipofika ofisini kwake, alimkuta marehemu ameketi kwenye kiti lakini alionekana dhahiri hali yake si nzuri kwahiyo aliuliza wale wasaidizi, kumetokea nini.
Wasaidizi wakasema hapana, alipofika hapa aliomba kiyoyozi kiongezwe ubaridi, kitu ambacho kilifanywa kisha akaketi kwenye kiti, kwahiyo katibu mkuu alifanya uratibu haraka wa magari pale na kumchukua marehemu Mfugale kumtia kwenye gari na kumkimbiza katika hospitali ya Benjamin Mkapa, wakati huo alifanya uratibu na katibu mkuu Afya ambae aliandaa madaktari ambao walipofika pale Benjamin Mkapa, walikuta wanasubiriwa na wakamchukua na kumkimbiza ili apate huduma stahiki.
Baada ya kufanya uchunguzi mfupi, walisema Mhandisi Patrick Aron Mfugale tayari amekwishafariki, baada ya hapo tulianza uratibu wa kuitafuta familia ili tuijulishe kabla ya taarifa nyingine kuifikie jamii.
PIA, SOMA=> Erasto Mfugale: Kilichotokea kazini sisi hatujui