Waziri Deogratius Ndejembi: Bilioni 163 zimetengwa ili kutengeneza ramani mpya ya Tanzania, magari 70 kununuliwa

Serekali imejaa mipango isiyotekelezeka kwa lengo lengwa isipokuwa uhakika wa kunufaika watendaji wa Wizara na Idara.
Tujikumbushe:
1. Lukuvi aliishawahi kuja na mpango kabambe wa mipango miji yote kwa mikoa yote....Hora!
2. Nepi Mnauye aliishawahi kusimamia uanzishwaji na uwekaji namba za mitaa na nyumba mitaani tena akiziangalia kwa makini kutoka ndani ya helikopter .... Hora! 😝
3. Edward Lowassa aliwahi kutoa kali zaidi, aliwahi kwenda mashariki ya mbali kutafuta utaalamu wa kutengeneza mvua..... Matokeo yake leo hii mvua inanyesha Dar!.
Du!! Nchi ya Futuhi sana hii hadi kichwa kinauma.... 😢
 
BADO MWEZI APRIL, MAY, JUNE, JULY, AUGUST, SEPTEMBER, NA OCTOBER; MPAKA KUFIKIA HIYO OCTOBER TUTASHUHUDIA MENGI, STAY TUNED
 
Hapa kuna dalili za upigaji. Open data source zipo nyingi ambazo unapata kila kitu. Sijui wanalenga kufanya kitu gani kipya?
Kama data wanazotegemea kufanya hazitafika level ya mtaa boundary kwa budget hiyo itakuwa ni upigaji.
Wahuni tu hawa

Ova
 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi, amesema wakati wa uzinduzi wa Sera ya Ardhi ya mwaka 1995, toleo la 2023, jijini Dodoma katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, kuwa maelekezo ya Rais Samia kuhusu upangaji na upimaji wa ardhi yamefanikiwa kwa kiwango cha juu zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Amesema katika utekelezaji wa maelekezo hayo, serikali imetoa takribani shilingi bilioni 50 ambapo Wizara ya Ardhi kwa kushirikiana na TAMISEMI zimezikopesha halmashauri zaidi ya 52 kwa ajili ya upimaji wa ardhi.

Pia, serikali iliridhia na kutoa bilioni 133 kwa ajili ya vitendea kazi mbalimbali vya kuboresha sekta ya ardhi, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa magari 70 ambayo yamekabidhiwa rasmi kwa Wizara ya Ardhi na Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika hatua nyingine, serikali imewekeza Dola za Marekani milioni 65 kwa ajili ya kutengeneza ramani msingi mpya ya nchi, jambo ambalo kwa mara ya mwisho lilifanyika mwaka 1978.
Acha Trump na Elon Musk watubane. Huo wote ni mchongo.
 
Nikishaona kiongozi yoyote amejivimbiavimbia tu (irregular structure), napigilia mstari kuwa kichwani ni {} set. Kwa hiyo huyu jamaa pamoja na watendaji wengine wa wizara wamefanya tafakuri ya kina na kuona kuwa ramani ya nchi ndio kipaumbele cha Watanzania kwa sasa katika sekta ya ardhi?
 
Back
Top Bottom