DOKEZO Waziri Dkt. Gwajima, fanya yafuatayo ili kuwakomesha wahuni (beach boys) wote katika fukwe zetu za Dar es Salaam

DOKEZO Waziri Dkt. Gwajima, fanya yafuatayo ili kuwakomesha wahuni (beach boys) wote katika fukwe zetu za Dar es Salaam

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
1. Tangaza haraka Kuzuia vile Vijiwe vyote vya Kukodisha Mapira / Matairi ya Kuogelea

2. Kisha amrjsha wanaotaka Kufanya hiyo Biashara Kwanza wajisajili Kwenu (Serikalini) na wekeni Ada / Tozo Kubwa ili kama kuna Watakaojitokeza basi wawe ni Watu Serious na siyo hawa Wahuni walioko

3. Kwa kila atakayejitokeza mlazimisheni awape Picha zake na mjua Makazi yake na taratibu zingine za Kiusalama dhidi yao zifanyike kama njia ya Kuwadhibjti.

4. Kuwe na Chama chao Beach Boys ambacho Kitatambulika nanyi Mamlaka na walazimishenj Wanachama wao (nikimaanisha Vijana wao Wanaofundisha Watu Kuogelea Baharini) wawe ni Watu very Professional na Ethical pia

5. Serikali (Mamlaka) iweke Matangazo katika Beach zote (tena yawe Makubwa) kuwa Mabinti / Wanawake ambao watafanyiwa Ukatili huo wapige Simu upesi kwa Mamlaka zenu ili Wahusika wakamatwe.

6. Himizeni kwa Beach Goers Wote hasa Wanawake / Mabinti kuwa kama wanataka Kufundishwa Kuogelea na Beach Boys basi wawachukue wale ambao ni qualified na kutoka sehemu husika.

7. Beach Boys wote watakaowepo iwe ni AMRI lazima wawe na Vitambulisho na Uniform ili irahisishe hata Kujulikana mapema wakifanya huu Uhuni wao.

8. Katika Beach zote wekeni Eneo Maalum (ndani ya Maji) la Watu Kufundishwa Kuogelea kwani moja ya Mbinu Kubwa itumikayo na hawa Wahuni (Beach Boys) ni kwenda na Wahusika katika Directions ambazo hakuna Watu Wengi na kwenye Kina Kirefu kisha wanafanya huo Uhuni wao.

9. Mkazo uwekwe zaidi kwa Watu Kujifunza Kuogelea katka Vituo Maalum au Shule za Uogeleaji (hasa Swimming Pools) ili basi wakiwa wanaenda Baharini wawe ni Wajuzi na siyo Watafuta kujua Kuogelea ambako hukutana na hawa Wahun

10. Tungeni Adhabu Kali na isiyo na Huruma dhidi yao ili Kulimaliza hili tatizo na kuleta Nidhamu katika hayo Maeneo husika (Beaches)

11. Ili Kuwakamata tumieni huu Mtego wa kuwatafuta Mabinti (Wanawake) Watatu tu ambao wanajua kweli Kuogelea au mkiweza Wachukueni wa pale Navy Kigamboni kisha Wapandikizeni katika kila Beach.

Wakiwa huko Wahimizeni wajifanye hawajui kabisa Kuogelea kisha wavalie Nguo za Kutamanisha na wawe Wanajibebjsha kwa hao Beach Boys.

Wakati mnapanga hili pia mnawapanga Watu (huku nchi Kavu) wakiwa na Camera za Ujasusi wanawachukua ili kuwa na Ushahidi very Vivid ambao hawataweza Kuruka.

Pia hakikisheni mnawatafuta Wavivu na Mitumbwi yao ili wakati mnazifanya hizi Oparesheni nao Wawe wanajifanya kama vile wako Baharini wanaendelea na Shughuli zao za Uvuvi.

Kisha hawa Mabinti / Wanawake ambao mtawapanga Wajirahisi kwa Beach Boys (ambao napendekeza lazima Wawe ni Wajuzi wa Kuogelea hasa) mtawaambia wakishaingia tu kwenye Maji na kupelekwa Maji Marefu na kuanza Kuombwa Ngono au kutaka Kubakwa upesi sana watoe Ishara kwa wale Wavivu mtakaowapanga watakaokuwa Eneo Jirani na kwa Askari wengine ambao mtakuwa mmewapanga huku nchi Kavu.

Mkishawakamata hawa Wachache watataja Mtandao wao Wote na Kutajana (huku mkiruhusu na Sisi Raia tuwatje Adabu kidogo kwa Vipigo vya kishalubela) pale pale Baharini ili kutoa Signal kwa Wenzao wengine kuwa sasa Serikali kwa Kushirikiana na Raia Wema (akina GENTAMYCINE) mmeamua / tumeamua Kuwadhibjti.

Na baada ya hapo tu mnaondoka nao kwenda Polisi ili kuanza taratibu zingine za Kisheria ila naomba Adhabu ya Viboko ama 6 au 12 isikosekane na Kifungo kirefu

12. Na katika Vijiwe vyao vyote hao Beach Boys huko Baharini baada ya Kuwasajili Kisheria kama nilivyoshauri hapo mwanzoni pia himizeni / lazimisheni kila Kijiwe kiwe na Utambulisho wa Namba na Jina Kubwa lililoandikwa

13. Ikiwapendeza himizeni / lazimisheni kila Binti / Mwanamke aendae Kuogelea Baharini aende na Pila / Tairi lake kutoka Kwao / Kwake kwani Wengi Wao wakati Mwingine hujikuta wanajngia Majaribuni hadi Kulalwa kwa Kukosa tu Vifaa hivi.

14. Tangazeni kabisa Binti / Mwanamke ambaye kwa Upumbavu na Uwoga wake bila kusahau Tamaa zake za Mwili akikubaliana na huu Uhuni wa hawa Wahuni Beach Boys na likampata la Kumpata asije Kulaumu Mtu au Serikali

15. Mwisho tengezeni Vipindi Maalum katika Redio na Television vya Kutoa Elimu na Kuonya juu ya Ukatii huu mkubwa huku mkihimiza kila Beach Goer (Mpenda kwenda Kutembea Baharini) awe ni Mlinzi wa Mwenzake pasipo kujali ni Ndugu yako au si Ndugu yako

Ni haya tu Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima D nakuomba yafanyie Kazi yote na GENTAMYCINE nakuhakikishia hapa hapa JamiiForums kuwa Tatizo hili utalimaliza na Kuokoa wengi.

Nimekuheshimu sana kwakuwa navutiwa na Utendaji wako mzuri wa Ushirikishaji wa Wadau na nakuahidi kukupa Ushirikiano zaidi kwa Mambo / Masuala mengine ya Kijamii ukihitaji kwani 97% ya Maisha yangu ya kila Siku ni kuwa na Jamii na kuwa na Uwezo mkubwa wa Kuchunguza Jambo, Kulifuatilia, Kulijua, Kulirekodi katika Ubongo wangu, Kulikabili Kifikra na Kimatendo na kutoa Suluhisho la Dharula, la Kati na la Kudumu.

Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima D tafadhali kama utakuwa na Zawadi yoyote ile Kwangu GENTAMYCINE (itakayokupendeza) kwa hiki nilichokuandikia hapa basi utakitangaza hapa hapa JamiiForums kisha utaipeleka katika Ofisi za JamiiForums Kawe Avocado na utampa JamiiForums Founder Mtani wangu wa Kihaya na Kaka Maxence Melo na yeye atajua wapi atanipata na Kuiwasilisha Kwangu kwa Niaba yako.

Na nikutoe Hofu Dada (Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima D) hata kama hutonipa Zawadi yoyote ile bado nakuhakikishia nitaendelea kukupa Ushirikiano wangu mkubwa bila Kinyongo na Usununu.

Kila la Kheri Mheshimiwa

Tupo pamoja.

Akhsante.

Wako GENTAMYCINE Nahodha wa Kudumu wa wana JamiiForums wote duniani.
At least umeongea point leo siyo zile ngojera zako za kina popat na kilufitini watu
 
Sasa ukahaba mbona hata kwenye biblia umetajwa, haujaanzia TANU. Upo kabla ya yesu.

Tena biblia ukiisoma raha sana, maana kuna kisa mule kuna kahaba anaitwa Tamari (unajuwa Tamari kwa Kiswahili ni nini?

Huyo Tamari alinishinda ukahaba kwa nilivyokisomakisa chake ndani ya Biblia, ana vituko na ana akili sana, na yeye yupo katika vizazi vya Yesu.

Apewe maua yake.
Kwenye ule uzi wako wa kutongozwa kulikuwa na mafanikio yoyote?
 
Hii lazima itaibwa kule kwenye magazeti halafu hawatatoa credit kwako mleta uzi wenye akili nyingi sana na madini adhim

Kongole Mkuu
Asante sana Mdogo wangu wa Damu kabisa steveachi hakika Marehemu Babu yetu alituachia Wajukuu zake Zawadi Kubwa ya Maarifa, Umakini na uwezo wake mkubwa wa Akili na Sisi Wajukuu zake Wapendwa tunapita mule mule tu.

Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake na za Marehemu Wapendwa Wetu wengine Wote mahala pema Peponi Amen.

Tuko pamoja Dogo.
 
Ushauri mzuri sana.

Ila juu ya swala la kutafuta NAVY kwa ajili ya kufanya operation ya kuwakamata wahuni wepesi kama hao ni kulishushia hadhi jeshi letu tukufu.

Isitoshe, operations za kijeshi zinaenda kwenye mambo mazito haswa. Si kwamba nadharau sana Unyanyasaji wa kijinsia unaotendwa na Beach Boys, ila ni jambo dogo sana likitiliwa maanani na vyombo husika. Polisi waamue tu kulivalia njuga.

Wataalam wa sheria watanisaidia na watanisahihisha. Kumshawishi mtu atende jinai ili uweze kumuwajibisha haitakiwi. Kwenye muktadha wa haki, atakushinda mahakamani. Ninachomaanisha, kuwachukua NAVY na kuigiza huku wakijirahisha sana kwa hao Wahuni kisha baadae wawatie nguvuni, haikubaliki. Ukusanyaji wa ushahidi ni jambo rahisi sana kwa vijana wa hovyo.

Vingine, umesema vema sana.
Mh Dkt. Gwajima D atayazingatia.
Uko sahih Sana jama angu kweny sheria Ni mweupe pee haujui kuwa kufanya hyo kuweka mtego ni kosa pia kisheriaa kumfunga mtu Ni Jambo rais

Otherwise mengine yanawezekana
 
Kwenye ule uzi wako wa kutongozwa kulikuwa na mafanikio yoyote?
Mengi sana, unadunda mpaka leo. Kauchungulie.

Si unaona, umeshindwa hoja yako ya uongo umehamisha magoli.

Mara mmeanza mdini, mkaja kahaba, sasa kutongozw. Mtamaliza nyimbo lakini hoja zangu zinabaki palepale.
 
@GENTAMYCINE, Nirudie tena kukushukuru kwa ushirikiano wako. Nimesoma btwn lines. Hapa nahariri action plan ya kujumuisha wadau wote huku nikijumuisha na haya maoni yako. Nikiri, kuna mashiko mazuri kabisa kwenye haya maoni yatakayochangia Hatua zetu na wadau. Hatua ya kwanza, napanga mazungumzo ya haraka na wadau wote tukubaliane twende mbele na utekelezaji wa haraka.

Huu ndiyo umoja wa kijamii. [emoji1241]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Asante sana Dada yangu Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima D kwa Kunielewa kwa niliyokuandikia, kuyakubali na kuahidi kuyafanyia Kazi haraka mno ili Kulimaliza rasmi.

Tuko pamoja Dada piga Kazi. Tunakupenda na Kukuthamini na ndiyo maana GENTAMYCINE nimeamua kukupa Ushirikiano wangu wote.

Una bahati sana na Mimi Dada.
 
Asante sana Dada yangu Mheshimiwa Waziri Dkt. Gwajima D kwa Kunielewa kwa niliyokuandikia, kuyakubali na kuahidi kuyafanyia Kazi haraka mno ili Kulimaliza rasmi.

Tuko pamoja Dada piga Kazi. Tunakupenda na Kukuthamini na ndiyo maana GENTAMYCINE nimeamua kukupa Ushirikiano wangu wote.

Una bahati sana na Mimi Dada.
Ila wewe jomba unajimwambafy hadi kwa waziri!!.. 😄😄😄 yaani waziri ndo kabahatika kwako kupata ushauri??
 
Mengi sana, unadunda mpaka leo. Kauchungulie.

Si unaona, umeshindwa hoja yako ya uongo umehamisha magoli.

Mara mmeanza mdini, mkaja kahaba, sasa kutongozw. Mtamaliza nyimbo lakini hoja zangu zinabaki palepale.
Wewe sio kwamba huna akili tatizo ni hiyo roho yako mbaya ya kigaidi uliyo nayo. Unautumia uislamu vibaya.
 
Samahani kama nitawakwaza Mwanamke anayebakwa Beach asilimia kubwa wanakuwa wametengeneza mazingira wenyewe..
 
Bila shaka ni muhaya
GENTAMYCINE ni 100% Zanaki ( Mara ) na 100% Yao ( Mtwara ) ila Mababu zangu walitokea Rwanda katika Kabila la Watutsi na wakaja huku Tanzania na Kuulizwa Wazanaki ( yaani mmekuja na nini ) na Wengine wakaenda Uganda wanaitwa Banyankole na Bahima huku wengine tena wakaenda Mkoani Kagera na wanaitwa Wanyambo ambapo Kenya pia wapo wanaitwa Kalenjin na Congo DR pia wapo wanaitwa Banyamulenge au Kadogoo. Pata Elimu hii ya bure iweze Kukusaidia.

Cc: steveachi, adriz, Glenn na Bujibuji Simba Nyamaume
 
Yaani huyu FaizaFoxy yy ana lake tu lingine na mimi. Ni fumbo la Imani. Wenzake wote wataona ila yy hapana. Ni kama ile Hadith ya wale 99 mmoja amepotea. Abarikiwe tu. Nishamzoea kama wengine walivyomzoea. Kaziiendelee...

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Mental Case huyo asikusumbue wala asikupotezee muda Dada. Piga Kazi na tuko nyuma yako na pamoja nawe.
 
Nimeshaanza ndugu yangu. Tukumbuke kuwa, kwenda kwenye jamii siyo wizara moja peke yake bali timu ya kisekta na mamlaka kadhaa kwa pamoja; Wizara hii ya Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Polisi, Wizara ya TAMISEMI, Wizara ya Biashara, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa uchache; nimeona nielimishe wadau Ili wajue kwa nini kuna wakati wengine wanaweza kuona mbona asitamke tu yeye? Kwa mujibu wa nyenzo za kazi na dhamana kuna utaratibu Ili kile kikitamkwa, kiwe sustainable na kimilikiwe na mfumo. Hivyo, mm sasa nawaratibu wenzangu wote twende pamoja. Tuwe na subira na tufuatilie.

Shukrani.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Nimekuelewa vyema kabisa Mheshimiwa Waziri. Asante Kwako pia kwa kuendelea Kulipigania na Kutuonyesha Ushirikiano wako bila Kuchoka. Ubarikiwe na udumu hapo Wizarani.
 
Dah, wanawake hampendani kabisa aisee
Na hasa Mmoja akiwa Mzuri kama Gari aina ya Mercedes Benz na Mwingine Mbaya kama Lorry la Mchanga BEDFORD ndiyo balaa kabisa katika Kupendana Kwao kama Jinsia moja.
 
Una chuki binafsi.
Huyu Gwajima d angekuwa muislam mwenzio hata angekuwa dhaifu ungemtetea na kumlinda.

Huna maana sasa dada FaizaFoxy .

Niambie ni waziri gani mwanamke ni mchapa kazi kumzidi huyu?
Akikujibu na Kumtaja kwa Makusudi ( bila Uwoga wa Kichapo na Adhabu ) naenda Kususu ( Kukojoa ) Getini MP 1 Jeshini Makongo Lugalo Mubashara mchana Kweupe....!!
 
Back
Top Bottom