Waziri Dkt. Nchemba azungumza na Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas Lyimo

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
DODOMA-Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA), Aretas Lyimo, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Mamlaka hiyo, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Bw. Andambike Mololo wa Wizara hiyo, Kamishna wa Utawala DCEA, Shaaban Khatib Baraza na Kamishna Msaidizi Mipango na Bajeti DCEA, Lusajo Gilbert .
 
Taarifa hii ilitakiwa itolewe na Lucas Mwashambwa na si mtu mwingine.
 
Kwani Ipo chini ya wizara yake au ashakuwa waziri mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…