ChingaMzalendo
Senior Member
- Nov 9, 2008
- 192
- 3
Hivi wakuu mtu akiwa na bachelor flani hivi hafai kuwa kiongozi mpaka awe na Masters au PhD feki?Kwa mfano mtu kama Mathayo David ana degree nzuri tu ya veterinary medicine lakini nae nasikia ana PhD la kufoji,sasa ina maana hiyo bachelor haimtoshi kuwa mbunge mpaka ahangaike kufoji udaktari wa falsafa?
Mimi huwa nawashangaa sana hawa wakulu tatizo nini?Kina Nchimbi,Mary Nagu,Mahanga nk tatizo lenu nini?[/QUOTE]
Title,...... Ujiko,...... Siunajua tena kibongobongo,........ninshomile!!!!
TCU ni hopeless, ukiwauliza vyuo gani vinafaa hawakupi jibu; ukiandika barua hawajibu, sasa unategemea nini!!!! Hizo degree hawajafoji bali wamezisomea kwenye hivyo vyuo ambavyo tunaita " feki".
Hili swala la viongozi wenye Shahada za kusuka liliwahi kujadiliwa hadi bungeni; Kama sikosei mheshimiwa Shelukindo ndiye aliyeanzisha mjadala huo na waziri Msola akaahidi kulishuhulikia lakini mpaka leo kimya!! Inaelekea wanamtandao ndio wengi wenye vyeti feki ndio maana hatua hazichukuliwi ipasavyo ukianzia na Nchimbi, Lukuvi, Makongoro. David Mattayo, Mzindakaya , Masaburi , Nangale etc. Jambo la kusikitisha ni kwamba usanii wetu tumeupeleka mpaka kwenye E.A. legislative assembly ambako wabunge wa wenzetu ni wasomi kweli kweli na ndio maana wanasema ukihiyo wetu ndio unatufanya tuogope soko la ajira Afrika Mashariki lisiwe huru !! Hii ni aibu, ni vizuri vyeti vya waomba uongozi mwaka 2010 vikahakikiwa na competent authority kabla ya kuruhusiwa kugombea ili tuondokane na aibu hii.
Silencer nae mtupu ka edit lakni hakuliona hilo.Lol Mod of a yearMahoni ndiyo nini!? 😕
Dr. Mathayo PHD yake kaifanyia kazi na kuna kipindi alikuwa pale Botswana akifundisha kabala hajaenda kutafuta utajiri(ubunge)
Mkuu Gembe, kama huna data usikurupuke kumtetea mtu. Unajua kilichompata Botswana au unajisemea tu? Kweli kafundisha Botswana, lakini hii haina maana kuwa Mathayo ana PhD ya kweli. Kule Botswana alidanganya kama anavyofanya sasa bongo. Alipoona dili linaanza kubainika, akatoroka kwa kisingio kuwa anakuja kutibiwa bongo. Hakurudi tena Botswana mpaka leo. Kulikuwa na tetesi kuwa alikuwa anatafutwa Botswana. Sijui sekeseke lile liliishia wapi! Alipofika bongo akajiingiza kwenye mchakato wa kutafuta ubunge kupitia ujanjaujanja wa uanamtandao. Jamaa ni mjanja sana, ubunge kaupata na uwaziri juu. Bahati mbaya sana vyombo vyetu husika Tanzania haviwajibiki mpaka vilazimishwe kufanya kazi (Agalia EWURA : Imejitutumua hivi majuzi baada ya kikwete kumwambia Ngeleja aibane EWURA kudhibiti mfumuko wa bei za mafuta nchini). TCU au chombo chochote husika kikiamua kufuatilia udokta wa Bw. Mathayo utaghundua kuwa Mathayo alipaswa sasa hivi kuwa keko na wala si kwenye cabinet au bungeni. Visingizio kibao, oooh hatuna meno, oohh, sheria ya kutupa mamlaka hayo haipo, ooh unajua hivi, oohh unajua vile, ooh, ....oohh....
Tena utaadabu, Mhe mweke kando kabisa na makundi yenu ya vyeti bandiaMsimsahau Dakitari Karume
Tena utaadabu, Mhe mweke kando kabisa na makundi yenu ya vyeti bandia
Taratibu mkuuTena utaadabu, Mhe mweke kando kabisa na makundi yenu ya vyeti bandia