#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

Askofu Gwajima hajaanza leo kuzungumzia masuala ya Chanjo, na mara ya mwisho alisema libaki suala la hiari ila yeye msimamo wake na wanaomfuata ni kuwa hawatochanja mpaka wathibitishiwe kilichopo kwenye chanjo. Akawa amemaliza na mjadaka ukaisha kila mtu ametua akili zake kuamua

Kitendo cha Waziri leo kutoa amri ya kukamatwa Gwajima ni dalili moja wapo za hujuma anazofanya kuzorotesha utoaji huduma za chanjo kwa kuendeleza mjadala, ubishani na sintofagamu, watu walishasikiliza wakang'amua waliomua kuchanja wakachanja waliokataa wamekataa anachofanya sasa ni kama kuirudisha tena sinema ile na kuendeleza sintofahamu hiyo makusudi

Leo hii Mama hayupo, anatoa amri shemeji yake ( kaka wa mume wake) akamatwe wakati hakuna kiongozi wa mkubwa yeyote wala wa vyombo vya dola aliyewahi kuagiza akamatwe kwa sababu ni suala la hoja. Tuko tunajadili mengine tunarudishwa nyuma tena mjadala wa Askofu Gwajima na chanjo

Kama unaona misimamo yako ya sasa inakinzana na uliyokuwa nayo utawala uliopita kaa pembeni, jiuzulu au nenda kamwambie Mama unaomba upumzike.
Mkuki kwa Chadema tu; kwa mwana-CCM la hasha. Akamatwe. Ni mchochezi.
 
mzigo unakaribia expiry date nn, mbona wamechanganyikiwa,,kuna Mangi fulani hua maziwa yake yakifika expiry date ana tabia ya kuzuga zuga,na kumbambikia mteja,usiposhtuka imekula kwako,serikali inataka kufanana na huyu mangi
 
Butiama.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ( Takukuru) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko 19.

Dk Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama akibainisha kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Credits: Mwananchi

Pia soma
- #COVID19 - Dkt. Mollel: Askofu Gwajima ataitwa athibitishe kauli zake, akishindwa tutamshughulikia
Sura ya huyu mama inadhihirisha kilichopo ndani ya mwili wake,
ROHO MBAYA
ASIYEKUBALI KUSHINDWA
SHOW OFF
MAJIVUNO
N.K.

Kama kwel Askofu ni shemeji yake basi akubali pia kutengwa na upande wa mume wake.
 
Butiama.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ( Takukuru) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko 19.

Dk Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama akibainisha kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Credits: Mwananchi

Pia soma
- #COVID19 - Dkt. Mollel: Askofu Gwajima ataitwa athibitishe kauli zake, akishindwa tutamshughulikia
Hilo lichizi likamatwe tu
 
Huyu waziri na naibu wake bora wafunge midomo yao tu wanatufanya sisi mazuzu kiasi tumepoteza uwezo si wa kuskia na kuona hata kunusa pia.

Hivi Hawa wananaga hata mshipa wa aibu kidogo?
 
Ngwajima ameagiza Gwajima akamatwe😝😝😝😝

Hawa watu wenye majina hayo bana inbidi tuwapime akili
 
Kujiita askofu ni kuchafua hadhi ya uaskofu, kuwa askofu kuna kanuni zake sio kujitangazia kiholela. Kamati iliyokaa na kumpa Gwagima uaskofu waliangalia sifa za uaskofu? Bila shaka hawakuangalia ndio maana anapayuka ovyo. Chungu ulimi wako mbele ya serikali.
Wewe Mzee wa MAMA ANAUPIGA MWINGI,hebu walau mjibu hoja za gwajiboy si kuleta udictator uchwara hapa
 
IMG_8481.jpg
 
Kwa hiyo hapo kwenye maneno ya mchungaji Gwajima kuna rushwa ya kuchunguza? hahahaha
Wao wanaamini gwajima kapewa rushwa apotoshe ila wao gwajima akisema wanaita polisi na Takukuru
 
Gwajima hana maadili na huo uasikofu wake ni utapeli tu,nashangaa Sana Kuna watu Bado wanamuamini Askofu tapeli.Yeye taaluma ya udaktari wa binadamu hana eti ndo anapinga chanjo ya korona kwa fake facts .Ina maana Gwajima ndo ana akili kuliko wanasayansi wote duniani aache uhuni wake.
 
View attachment 1895491Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ( Takukuru) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko 19.

Dk Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama akibainisha kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo. (Mwananchi)
Inashangaza mtu 1 anaeongea kwa wiki x1 anawashinda watu wote serikal mnaoongea kila siku?? Hv hi Ni akili kwel?? Hoja hukibiwa kwa hoja Kama anapotosha waweke ukwel fulstop, wasipofanya hvyo wao mdo wanapotosha...
 
Gwajima hana maadili na huo uasikofu wake ni utapeli tu,nashangaa Sana Kuna watu Bado wanamuamini Askofu tapeli.Yeye taaluma ya udaktari wa binadamu hana eti ndo anapinga chanjo ya korona kwa fake facts .Ina maana Gwajima ndo ana akili kuliko wanasayansi wote duniani aache uhuni wake.
Una mzungumzia gwajima yupi?Yule wafuasi na viongozi wa Chadema walokua wanakesha na kusali kwake huku wakiburudika na mahubiri yake au yupi?
 
Kujiita askofu ni kuchafua hadhi ya uaskofu, kuwa askofu kuna kanuni zake sio kujitangazia kiholela. Kamati iliyokaa na kumpa Gwagima uaskofu waliangalia sifa za uaskofu? Bila shaka hawakuangalia ndio maana anapayuka ovyo. Chungu ulimi wako mbele ya serikali.
Kaa kimya wewe huelewi!
 
Inashangaza mtu 1 anaeongea kwa wiki x1 anawashinda watu wote serikal mnaoongea kila siku?? Hv hi Ni akili kwel?? Hoja hukibiwa kwa hoja Kama anapotosha waweke ukwel fulstop, wasipofanya hvyo wao mdo wanapotosha...
Sukumiza ndani Gwajima, mengine yatajulikana mbele ya safari
 
Back
Top Bottom