#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

Kujiita askofu ni kuchafua hadhi ya uaskofu, kuwa askofu kuna kanuni zake sio kujitangazia kiholela. Kamati iliyokaa na kumpa Gwagima uaskofu waliangalia sifa za uaskofu? Bila shaka hawakuangalia ndio maana anapayuka ovyo. Chungu ulimi wako mbele ya serikali.
Gwajima ni mhuni tu Hana maadili kwa nchi ambazo Zina sheria za maadili huyu jamaa hakifaa kuwa mbunge,na pia ni tapeli na mlaghai ashandanganya anafufua watu ,rejea kisa cha Amina chifupa.Inaskitsha sn Kuna watu Bado wanamuamini.
 
Wampeleke mahabara ya taifa kwenye kila aina chemical na kifaa atakachohitaji kwenye test zake athibitishe madai yake ili asiseme kaonewa bila ya kusahau na kichupa kimoja cha vaccine.

Akifika huko achanganye hayo madawa mbele ya camera kuthibitisha madai yake kwa umma nini kimo ndani hiyo vaccine kama anavyodai.

Bishop Gwajima anavuka mipaka yake.
 
Inashangaza mtu 1 anaeongea kwa wiki x1 anawashinda watu wote serikal mnaoongea kila siku?? Hv hi Ni akili kwel?? Hoja hukibiwa kwa hoja Kama anapotosha waweke ukwel fulstop, wasipofanya hvyo wao mdo wanapotosha...
Akili mbovu ni wapuuzi kuamini uzushi na upuuzi wa Gwajima wa verse moja

dr Gwajima katenda haki
 
Una mzungumzia gwajima yupi?Yule wafuasi na viongozi wa Chadema walokua wanakesha na kusali kwake huku wakiburudika na mahubiri yake au yupi?
Namzungumzia Asikofu Rashidi Josephat Gwajima mbunge wa Kawe.
 
Kuna wakati kwa sababu ya madaraka na mtu kutaka kujionyesha wewe ni nani hasa, ndio huwafanya wengi kuishia kuwa vituko badala ya kulinda heshima yako na kutambua wewe ni mtu uliyepo kwenye nafasi hiyo ni psmoja na kutoa majibu ya maswali ya watu unaowaongoza

Kumkamata Askofu Gwajima, ni hasira za kiongozi anayeshindwa kujibu maswali ya Askofu Gwajima

Gwajima hapingi Chanjo ispokuwa anataka majibu tu kutoka wizara husika, Je, Yeye Waziri akiulizwa, Kipindi cha hayati alikuwa akisimsmia nini na sasa anasimamia kipi, hilo nalo ni kosa kuulizwa hivyo, viongozi wetu msipokuwa wavumilivu na watu wa kutafuta majawsbu ya watu mnaowaongoza, mtawachunguza wote wanaowaulizeni
 
Leo hii Mama hayupo, anatoa amri shemeji yake ( kaka wa mume wake) akamatwe wakati hakuna kiongozi wa mkubwa yeyote wala wa vyombo vya dola aliyewahi kuagiza akamatwe
Hata kama mama hayupo nchini haina maana kwamba hawezi kufanya kazi za nchi yake.

Waziri Gwajima hawezi kufanya maamuzi ya kumkamata mbunge wa ccm bila mama ama wakubwa wengine kujua/kumpa maagizo.
 
Butiama.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ( Takukuru) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko 19.

Dk Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama akibainisha kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Credits: Mwananchi

Pia soma
- #COVID19 - Dkt. Mollel: Askofu Gwajima ataitwa athibitishe kauli zake, akishindwa tutamshughulikia
Huyu Mama akirudi kwa Mumuwe atachapwa sana viboko na Mumewe,unampelekaje Shemeji yako police!? Je ulimshitakia kwa Kaka yake Kwanza!?
 
Back
Top Bottom