#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

Askofu Gwajima ni shemeji yangu, lakini mimi waziri wa wananchi nimekula kiapo mbele ya Rais cha kutumiakia nchi, sio kumtumikia shemeji. Mimi ndiye msemaji wa masuala ya afya nchini, nimechoka kuvurugwa naagiza akamatwe popote na akahojiwe juu ya haya madai - Dk. Gwajima...
Nailaumu mno MOSSAD ya Mzizima kwani imemchelewesha sana huyo Gaidi na Tapeli wa Kiimani Tanzania.
 
Nailaumu mno MOSSAD ya Mzizima kwani imemchelewesha sana huyo Gaidi na Tapeli wa Kiimani Tanzania.
Unaweza kueleza ni kwanini akamatwe?

Serikali imesema chanjo ni hiari na Gwaji anaeleza wasiwasi wake juu ya chanjo kosa liko wapi?

Kwanini msijibu kujibu hoja kwa hoja?

Mna vichwa vya panzi hamuwezi kujibu hoja.

Hamna tofauti na mkoloni...phaller wewe
 
DHULMA HAIDUMU NA ENDAPO ITADUMU BASI ITA ANGAMIZA.

Nimeamini
 
Rais hawezi kusoma ripoti, kuwaza nje ya boksi acha apelekeshwe. How come anasema Tanzania ni nchi jirani na marekani? unaona kuna mtu humo mkuu.
Leta ushahidi wa yeye kutamka haýo maana wote tulimsikia na hakusema hivyo unamlisha maneno
 
Tukifuata sheria, ni kweli Mbunge Gwajima hawezi kusema kuwa mawaziri hakupigwa chanjo, bali ilikuwa chanjo za kugeresha, waziri ama serekali ina haki ya kutaka uthibitisho kwa huyo Mbunge, na njia ya sheria ni polisi kumuita na kumhoji, akikataa kwenda kwa hiari yake basi nguvu ya dola ni wajibu itumike.

Serekali haipaswi kuwaogopa hawa watu wanao kiki ya umaarufu kwa kutumia uongo.
 
Anakamatwa then what? Intimidation tactics za kindezi sana hizi.

Si wamburuze mahakamani directly akawahoji/wakamhoji vizuri? Na labda hicho ndicho Gwajima anakitaka na hawa wameingia kichwakichwa
Anajua hawamuwezi
Ngoja tuone mwisho wake
 
Ndungae yuko mbioni kulitangaza jimbo la Kawe kuwa wazi. Aliyekuwa anashika jimbo hilo kaondokewa na sifa za kuwa mbunge. Sasa haijajulikana kama Halima Mdee atagombea tena jimbo hilo hata kwa kupitia mlango wa ACT - Wazalendo maana mlango wa chadema hauna ufunguo. Mwenye ufunguo yuko mahabusu ya magaidi.
 
gwajimapic.jpeg


Hoja za Dk Dorothy Gwajima kuhusu kuagiza kukamatwa Gwajima

- Mara kadhaa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha juu ya chanjo na hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi yake, jambo ambalo limekuwa likileta mkanganyiko katika jamii.

- Sekta ya afya si ya kuchezewa, hivyo yeyote atakayejaribu kupotosha au kuvuruga mipango ya Serikali ni lazima achukuliwe hatua bila kujali nafasi yake au uhusiano wake na mtu yeyote.

- DK Gwajima amesema Askofu Gwajima amekuwa akidai kuwa chanjo zilizoletwa nchini ni feki, hivyo ni vema aeleze chanjo feki ziko wapi.

- Mambo ya sayansi yanapingwa na sayansi, hivyo Askofu Gwajima anatakiwa kutoa uthibithisho wa kisayansi juu ya madai yake hayo, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
"Gwajima ni ndugu yangu, ni shemeji yangu kabisa, lakini mimi ni waziri nimekula kiapo cha kutumikia nchi yangu sio kumtumikia shemeji yangu. Mimi ndiye msemaji wa masuala ya afya nchini, nimechoka kuvuruguwa. Naagiza akamatwe popote alipo ahojiwe juu ya haya madai yake na hatua zichukuliwe"

"Watu wanasema mbona chanjo imepatikana haraka wanasahau kuwa haya mambo ni ya kisayansi, nawaomba tuukatae ugonjwa huu katika jamii kwa kukubali kuchanja, wakati wataalamu wakiendelea na tafiti kwa ajili ya chanjo ya magonjwa kama ukimwi, malaria, TB na mengine,

“Nipo tayari kwenda kwa mkemia mkuu ili kupima chanjo itakayoonyeshwa na askofu huyo, ili kuthibitisha na endapo hatakuwa na imani na mkemia wa Serikali, wizara ipo radhi kwenda hata nchi jirani kwa ajili ya kupima chanjo hizo,” amenukuliwa Dk Gwajima.
 
Butiama.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kupambana na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kumkamata na kuhoji mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima ili athibitishe Tamko lake la kuzuia dhidi ya Serikali na kumbukumbu kuhusu chanjo ya Uviko 19.

"Gwajima ni ndugu yangu, ni shemeji yangu kabisa, lakini mimi ni waziri nimekula kiapo cha kutumikia nchi yangu sio kumtumikia shemeji yangu. Mimi ndiye msemaji wa masuala ya afya nchini, nimechoka kuvurugwa. Naagiza akamatwe popote alipo ahojiwe juu ya haya madai yake na hatua zichukuliwe "amesema"

Amesema mara kadhaa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa ya kupotosha juu ya chanjo na hakuna hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi yake, jambo ambalo limekuwa likichanganywa na mchanganyiko katika jamii.

Amesema sekta ya afya si ya kuchezewa, hivyo kila mtu anayejaribu kupakua mipango ya Serikali ni lazima achukuliwe hatua bila kujali nafasi zake au uhusiano wake na mtu yeyote.

DK Gwajima amesema Askofu Gwajima alikuwa akidai kuwa chanjo zilizoletwa nchini ni feki, hivyo ni vema aeleze chanjo feki ziko wapi.

"Nipo tayari kwenda kwa mkemia mkuu ili kupima chanjo itakayoonyeshwa na askofu huyo, alihakikisha na endapo hatakuwa na imani na mkemia wa Serikali, wizara ipo radhi kwenda hata nchi jirani kwa ajili ya kupima chanjo hizo," alisema Dk Gwajima.

Amesema mambo ya sayansi yanapingwa na sayansi, hivyo Askofu Gwajima anatakiwa kuthibitisha juu ya juu ya madai yake hayo, vinginevyo hatua Kali zichukuliwe dhidi yake.

"Watu wanasema mbona chanjo imepatikana haraka wanasahau kuwa haya mambo ni ya sayansi, naomba tuukate ugonjwa huu katika jamii kwa kukubali kuchanja, " alisema.
 
Takukuru wanaingiaje hapa? ina maana kila "jinai" ina rushwa?

Siku hizi muingiliano wa majukumu kati ya polisi na Takukuru ni mkubwa sana
 
Mimi watu wanaomsikiliza askofu Gwajima na kumuamini nawahurumia sana na wanaomsikiliza waziri Gwajima na kumchukulia serious nawahurumia zaidi
 
Back
Top Bottom