Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 242
- 1,141
Ameandika Dkt. Gwajima D katika Mtandao wa X.
Ndugu Wananchi, nimepokea 'Tags' nyingi za maoni na maswali kuhusu taarifa iliyotolewa na RPC mkoa wa Dodoma juu ya mwenendo wa shauri la 'Binti wa Yombo' (reja taarifa za awali).
Ndugu Wananchi, nimepokea hisia zenu, maoni na maswali yenu ambayo mmeelekeza kwangu. Nimewasiliana na Mhe Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye tayari naye amepokea na anafanyia kazi hivyo, tumpe nafasi atatoa taarifa yake.
Ndugu Wananchi, ni dhahiri kuwa, alichofanyiwa 'Binti wa Yombo' ni kitu kibaya kisicho cha utu hivyo, anastahili haki yake kwa mapana yote.
Ndugu Wananchi, Nawasihi tujipe muda na kuamini kuwa, haki itatendeka kwa mujibu wa sheria na itaonekana bayana na siyo vinginevyo.
Pia soma: Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza