Pre GE2025 Waziri Gwajima ashauri Siku ya Wanaume itambuliwe rasmi Tanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia,wanawake na makundi maalum Doroth Gwajima amesema kuwa serikali inampango wa kuifanya siku ya wanaume duniani 19 november kuwa rasmi kwa maadhimisho ya siku hiyo.

Dkt Gwajima ameyasema hayo mkoani Geita katika kongamano la kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani ambapo kanda ya ziwa yamefanyika wilayani Bukombe ikihusisha mikoa sita katika kanda hii.

Gwajima alesema kuwa kutokana na wanaume kuwepo kwenye sera ya ushirikishwaji ili waweze kuelewa lengo la ushirikishwaji wa mwanamke katika ngazi ya kiuchumi kupitia siku ya wanaume sasa wataelewa namna ya kumuwezesha mwanamke.

Soma, Pia: Singida kusherehekea siku ya wanawake duniani kwa kugawa mitungi ya gesi

Kongamano la wanawake wa kanda ya ziwa linalenga kumuinua mwanamke kiuchumi huku riba kubwa katika mikopo ikitajwa kuwa janga kubwa ambalo linamdidimiza mwanamke na kushindwa kuendelea kiuchumi.

Aidha katika hatua nyingine wanawake wamelipokea suala hilo la maadhimisho ya sikuya mwanaume kitaifa ambapo wamelitafsiri kama kuja kuwa njia bora ya kutoa elimu kwa wanaume juu ya ukatili dhidi ya mwanamke na kumuwezesha mwanamke

Wanawake wanasemaje kuhusu hili?
siku hizi akili zimeanza kuwarudia, sasa hivi posts nyinghi kwenye social media ni wanawake wakiwakubali wanaume na kuwasihi wanawake wenzao wajifunze kuwaheshimu wanaume, naona taratibu HESHIMA inaanza kurudi.
 
Yupo mmoja tu mwenye video zake mia nne

Wengine bado
 
Wanaume hatuna siku na inatakiwa isiwepo maana tutaanza kutetewa na hiyo sio nzuri kwa mwanaume.
 
Haya mambo ya siku na mwezi sisi huwa hatunaga, kila siku ni siku yetu............hebu tutoleee huo utumbo.
 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema kuwa serikali ina mpango wa kuifanya Siku ya Wanaume Duniani, inayoadhimishwa kila tarehe 19 Novemba, kuwa rasmi kwa maadhimisho nchini.

Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo Machi 02, 2025 mkoani Geita katika kongamano la kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa Kanda ya Ziwa, yaliyofanyika wilayani Bukombe na kushirikisha mikoa sita ya kanda hiyo.

Amesema kuwa wanaume ni sehemu muhimu ya sera ya ushirikishwaji, hivyo kupitia maadhimisho ya Siku ya Wanaume, watapata uelewa mpana wa dhima ya kumwezesha mwanamke kiuchumi na kijamii.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Geita ,Martine Shigela amesema ni vyema kwa taasisi za fedha kuona uwezekano wa kupunguza riba kwa vikundi vya wanawake au kwa mwanamke mmoja mmoja kutoka na na kundi hilo limekuwa na uaminifu katika suala la kurejesha kile wanachokopeshwa.

Aidha, baadhi ya wanawake wamepokea vyema wazo la kuadhimisha Siku ya Wanaume kitaifa, wakieleza kuwa linaweza kuwa njia bora ya kutoa elimu kwa wanaume kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia na umuhimu wa kumwezesha mwanamke katika nyanja mbalimbali za maisha.

Kongamano hilo limejikita katika kuwezesha wanawake kiuchumi, huku changamoto ya riba kubwa katika mikopo ikitajwa kuwa moja ya vikwazo vikubwa vinavyowakwamisha wanawake katika maendeleo ya kiuchumi.

View attachment 3257430
Kwamba tutaanza kuvaa sare? 😆😆
 
Muhimu tu isiwe public holiday; tunatakiwa kua na siku nyingi za kufanya kazi badala ya kua na siku nyingi za mapumziko; hata hivyo, haitakua na vibe kama hizo siku za wanawake, imagine siku zetu za kuzaliwa tu huaga hatukumbuki, ije hi? 😠 😡
 
Tutakoma singlemoms itakuwa ni malalamiko tu sikuhiyo🥴🙌
 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema kuwa serikali ina mpango wa kuifanya Siku ya Wanaume Duniani, inayoadhimishwa kila tarehe 19 Novemba, kuwa rasmi kwa maadhimisho nchini.

Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo Machi 02, 2025 mkoani Geita katika kongamano la kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa Kanda ya Ziwa, yaliyofanyika wilayani Bukombe na kushirikisha mikoa sita ya kanda hiyo.

Amesema kuwa wanaume ni sehemu muhimu ya sera ya ushirikishwaji, hivyo kupitia maadhimisho ya Siku ya Wanaume, watapata uelewa mpana wa dhima ya kumwezesha mwanamke kiuchumi na kijamii.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Geita ,Martine Shigela amesema ni vyema kwa taasisi za fedha kuona uwezekano wa kupunguza riba kwa vikundi vya wanawake au kwa mwanamke mmoja mmoja kutoka na na kundi hilo limekuwa na uaminifu katika suala la kurejesha kile wanachokopeshwa.

Aidha, baadhi ya wanawake wamepokea vyema wazo la kuadhimisha Siku ya Wanaume kitaifa, wakieleza kuwa linaweza kuwa njia bora ya kutoa elimu kwa wanaume kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia na umuhimu wa kumwezesha mwanamke katika nyanja mbalimbali za maisha.

Kongamano hilo limejikita katika kuwezesha wanawake kiuchumi, huku changamoto ya riba kubwa katika mikopo ikitajwa kuwa moja ya vikwazo vikubwa vinavyowakwamisha wanawake katika maendeleo ya kiuchumi.

View attachment 3257430
Tunaikaribisha tupikiwe ubwabwa!
 
Serikali ipitishe hii iwe siku maalum kwa wanaume wote waliochepuka na kukamatwa bahati mbaya wasamehewe na wake zao kwani hawatakamatwa tena maana kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa.
 
Back
Top Bottom