John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amewapongeza Ngariba walioacha kufanya ukeketaji na kugeuka kuwa wanaharakati wa kukemea vitendo vinavyo dhalilisha utu wa mtoto wa kike na kumuachia maumivu makali.
“Tuwavushe mabinti zetu kutoka usichana kuwa mwanamke bila madhara kiafya, mfano tuwape elimu, ukeketaji hapana una madhara tuache. Kila mmoja apaze sauti.
“Ukeketaji unakiuka haki za binadamu na pia kuna madhara makubwa kiafya, ndugu wote tuikatae mila hii, Tanzania imeamua kuukataa ukatili, mzazi epuka na kata kumkeketa mtoto wako,” - Dkt. Dorothy Gwajima